Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Kwa muda mrefu nimekaa na kutafakari sana hiki kinachoitwa laana juu ya uzao wa mtu fulani kina maana gani hasa na ni kwanini iwe ni adhabu kwa afanyae dhambi ili hali ameshondoka duniani ila kizazi chake ndio kitateseka.
Kwa mtazamo wangu, jibu rahisi hapa ni kuwa, unapotenda uovu kwa wanadamu wenzako na Mungu akakushushia laana kwako na kwa kizazi chako, maana yake ni kuwa, hata wewe utapokufa, utaendelea kuishi na kuona mateso uliowasababishia wanao, wajukuu zako, vitukuu wako, n.k. Na hiyo kwako hiyo inakuwa ni adhabu nyingine baada ya kuondoka hapa duniani kwa maana ya kuishi ukishuhudia mateso ya kizazi chako.
Ujumbe: Wale wenye mamlaka na mnaotumia madaraka yenu kutesa, kuumiza, kuua na kunyanyasa wengine, mjue mko katika hatari ya kuja kushuhudia mateso kwa uzao wenu baada ya nyinyi kuwa mmeondoka duniani ila mkiwa hai katika ulimwengu mwingine.
Last but not least, tusiogope kufa kwani inawezekana kabisa kuna maisha mengine nje ya huu ulimwengu ila cha msingi iishi vizuri hapa duniani.