Huu umaskini ni wa kutisha

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
133
379
Habari za mchana ndugu zangu,

Kuna dada mmoja alikuja home kutafuta chumba cha kupanga tukamuonesha chumba kimoja akakisafisha kesho yake akaja na mumewe kumuonesha.

Mume akadai chumba hajakipenda wakaondoka baada ya week akarudi tena, kile chumba kikawa kimepata mteja tukamuonesha chumba kingine.

Akasafisha akahamia jioni, jambo lililonifikirisha ni umaskini alionao huyu mama. Imagine ana watoto wanne hana kitanda wala gogoro yani yeye pamoja na mumewe na watoto wanalalia mkeka hata stuli moja tu hamna, ni nguo na vyombo vya ndani tu.

Najiuliza mumewe alikua na jeuri gani ya kukataa chumba kile wakati yeye hana kitu ndani.

Dunia ina maajabu hii, mume mlevi wa kutupwa dah poleni kina mama.
 
Watu wanaoishi hivyo nchi hii ni wengiii mnooo. Kumbe hujaona mengi, siku moja pita hata Kariakoo saa 8 usiku ujionee, watu wanalala kwenye mabox ya kukodi pembeni kwenye maduka ya watu kwa gharama ya Tsh 400.

Pita pita Dar usiku ujionee watu wanaolala barabarani.

Nchi hii ni ina hohe hahe wa kiwango cha kutishaaaa.
 
Watu wanaoishi hivyo nchi hii ni wengiii mnooo. Kumbe hujaona mengi, siku moja pita hata Kariakoo saa 8 usiku ujionee, watu wanalala kwenye mabox ya kukodi pembeni kwenye maduka ya watu kwa gharama ya Tsh 400...
Tatizo wanatoka mikoani kuja kubanana dar NA HAWANA HATA LAMANI NA PAKULALA eti wanasema one day watakuwa na maisha MAZURI

Wakati kwao wameacha nyumba na kitanda n.k

WARUDI KWAO.
 
Habar za mchana ndugu zang
Kuna dada mmoja alikuja home kutafuta chumba cha kupanga tukamuonesha chumba kimoja akakisafisha kesho yake akaja na mumewe kumuonesha...
Anapata pesa ya culera lakini sio ya kununua kitanda!!! kupanga ni kuchagua
 
Awamu ya nne
Na makando kando ya awamu ya nne, si mliyapigia sana kelele kamanda? maana awamu ya IV ilikua na matajiri sana, na masikini sana na kutishana tu mitaani "Unajua Mimi ni nani ?"

Au ndio tunasubiri kusifia tawala ikipita tayari?
 
Back
Top Bottom