architect astely
Member
- Nov 21, 2015
- 34
- 13
Ndugu wanajamii forum,nimechukua mda kutafakari haya matukio ya ujambazi yanayoendelea kutokea hapa nchini kwetu,tukiyachunguza kwa idadi ni matukio mengi ndani ya mda mfupi na raia kadhaa washapoteza maisha.Napenda nitoe rai kwa serikali na vyombo vya usalama vya nchi yetu kwamba kwa sasa inabidi hili jambo waliangalie kwa namna tofauti na sio tu ujambazi wa kawaida nikiwa na maana kuwa walishughulikie kama janga la taifa.Nikitoa mfano tu wa tukio la ujambazi lililotokea jana huko mbagala inasemekana majambazi walikuwa kumi na walikuwa wamejipanga vizuri wakiwa na bunduki na mabomu pia,je hao walikuwa ni majambazi tu wasaka hela ya starehe au ni kikundi fulani cha ugaidi kinachotafuta pesa za kununua silaha na kuweza kukuza mtandao wao?.Serikali inabidi ifahamu kuwa ata mbuyu ulianza kama mchicha,Al shabab na Isis hazikuanza tu kama makundi makubwa bali yalitokea hukohuko kwenye vikundi vidogo vidogo vya ujambazi,Na vile vile serikali ijiulize hao majambazi bunduki na mabomu wanatoa wapi?Samaki mkunje angali mbichi na hayawi hayawi yakaja yakatokea,Serikali na vyombo vya usalama komesheni hivi vikundi.Raia tunahitaji kuishi kwa amani katika nchi yetu.