Huu uchakachuaji ni kwa manufaa ya nani?

zaratustra

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
848
223
Leo asubuhi kama saa moja kasoro dakika kama kumi hivi, nilitaka sana kujua kilichoandikwa kwenye magazeti ya leo! bahati mbaya nika-tune TBC-1 (nimeandika: "kwa bahati mbaya" maana sina mazoea nao!). Baada ya bibie Amina Mollel kusoma kurasa za mbele, ndipo alipogeuza kurasa za nyuma, mahsusi kwa ajili ya michezo na burudani. Ndipo hatimaye akageukia magazeti maalum kwa ajili ya michezo akianza na gazeti la Bingwa.
Hapo ndipo nilishikwa na mshangao! Yaani huyo bibie alisoma gazeti la Bingwa lililotoka siku ya Alhamisi! Sasa, sikuelewa ilikuwa ni recorded au waliamua kuchakachua ama pengine walikuwa wanaangalia umakini wa watazamaji iwapo wanafuatilia matangazo yao au la!
Ila kwa kweli nilifedheheka sana kuona kituo cha TV kinachoendeshwa kwa kodi za waTZ, kinavyofanya mambo ya kipuuzi kama hivi!
 
It is sad and pathetic mkuu but hakuna cha kushangaza kupita kiasi maana hakuna umakini na kazi from top, to institutions, till to lower levels. Ingekuwa nchi za wenzetu wa Magharibi yaani hiyo ingekuwa ni scandal...imagine how many grave mistakes they make unnoticed
 
Back
Top Bottom