Wana JF kwa waliobahatika kuangalia kipindi cha Take One kinachorusha na kituo cha Tv cha Clouds jana tarehe 24/July kwa yale niliyoyaona nadhani kwa wenye taaluma ya uandishi wa habari watakubaliana na mimi.Kuna jambo nadhani kwa maono na fikra zangu sio la kiutu kwa kweli,kwa wale ambao hawakubahatika kuangalia naomba niwaelezee japo kwa ufupi,-Kuna msichana aliyetoka Dodoma na kuja Dar kuja kutafuta kazi na ndoto yake ilikua aje awe muugizaji,kutokana na maelezo yake aliyoyatoa alipokua akihojiwa na Zamaradi ambaye ndiye Host wa kipindi hiki,anasema alipewa nauli ya kuja dar na mama yake mzazi na alipofika dar alishukia Ilala ambapo kutokana na maelezo yake aliambiwa ndipo wanapoishi wasanii wengi aliopata kuwaona kwenye baadhi ya filamu za kitanzania,basi alipofika alipata mahali kwa mzee mmoja ambaye inasemekana kazi yake ni mlinzi,alikaa pale kwa muda na mzee alimsaidia kwa chakula,ilifika kipindi yule mzee akawa anamtaka kimapenzi hata ikafikia yule mzee kumwonyesha sehemu zake za siri,ikabidi ahame na kutafuta kazi kwa mtu.
Baadae akawa anaishi sinza na wasichana ambao inasemekana walikua wanafanya kazi ya kujiuza.Walimshawishi naye kujiingiza kwenye biashara hii ambayo ndio ilikua inampatia riziki yake,kutokana na taarifa yake alishiriki tendo la ndoa na wanaume zaidi ya 20 na wengine bila kinga.Na anasema wale wasichana walimlazimisha,imefika kipindi sasa anataka kwenda kucheki afya yake na anasema mmoja ya wanaume aliowahi kushiriki naye tendo la ndoa ni muathirika,alielezea kwa majonzi na masikitiko kweli na alikua anasema asingependa mamake ajue hili.Msichana mwenyewe bado ni mdogo anasema ana umri wa miaka 17.
Kilichonifanya niandike hili ni jinsi walivyomwonyesha msichana huyu ,nadhani kama mtayarishaji wa kipindi hiki alipaswa kutoonyesha sura yake,tumeona masuala kama haya ni ya kinyanyasaji kijinsia kwani walipaswa kutomwonyesha sura yake,hii inamuweka kwenye mazingira hatarishi zaidi kwani wale ambao amekua nao kwa mfano alisema alilazimisha kufanya nao mapenzi wanaweza kumdhuru na pia kimaadili sio vizuri kwani wapo watu wa umri na jinsia kama yake ambao nao inaweza kuwaadhiri.Lingine ni yeye kutotamani mamake kumwona na kujua alichofanya.
Maskini ndoto zake iliikua aje dar kutafuta maisha kwani mama yake na mdogo wake ndio wanamtegemea yeye lakini amejikuta akiishia kwenye maisha ambayo hakutegeme.Nifundisho ndio alikua anatoa kwa wengine ambao nao labda ndoto zake ni kama zake lakini kwa jinsi ilivyoonyeshwa nadhini sio Ki UTU na KIMAADILI,Tumekua tukiona kwa mfano wale waliobakwa au kufanyiwa ukatili wa namna kama hii wakionyeshwa kwenye vyombo vya habari bila sura zao na hata majina yao kutoonyeshwa lakini kwa hii ilikua tofauti.Naomba kama kuna wahusika wa haki za binadamu na wanaojua kuhusu hili waone jinsi wanaweza kulichukulia sheria ili lisiweze kutokea tena au hata kama ni funzo walikua wanatoa waangalie jinsi ya kuwakilisha jambo kama hili kwenye jamii.