Huu sasa ni uonevu!!!!

sir mweli

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
495
1,000
Habari wadau,

Leo nimetoka zangu job, nikasema nipitie kwa jamaa nlimwachia kazi anibanie CD ya nyimbo za Manton..Nimefika pale jamaa bado ajamaliza, basi nikasema nikae nisubirie maana nyimbo nyingine alikuwa hana hivyo inabidi azidanlod.....

Tumekaa pale mara wakaja polisi kama 11 wenye gwanda na waliovalia kiraia wakiwa na mitutu ya bunduki......Mara wakavamia pale , wanamwambia jamaa anafanya biashara kwa kukwepa kodi, sjui hana leseni....Mara wakaaza kuchkua Cd zake wanaeka kwenye mfuko.....wanachkua computer, subwoofer yake na vikorokoro vingine....

Kilichoniumiza zaidi jamaa wa watu mpole hata kuongea hajui.....naona ananong'ona tu mwenyewe kimya kimya sjui ndo alikuwa anasali......yaan nlichiskia anamwagiza jamaa tu kuwa amtaarifu mke wake kuwa amekamatwa.....Basi jamaa wakamchukua.....Sasa maswali kadhaa yakabaki yananiumiza kichwa..

1. Wanasema anakwepa kodi kwa kuingiza nchini bidhaa bila kulipia kodi, je huyu mwenye vi CD yake hata ishirini havifiki kweli anaweza kuingiza Mzigo toka Nje? Nnavyojua mm hawa wananunua kwenye maduka ya jumla kariakoo ambako kule wanapewa risiti ya TRA kuonesha wamelipia kodi....

2. Jee hao wanaoingiza hizi CD maana c za kibongo ni za Nje, si wanapitishia Mzigo bandarini?....na si wanalipa kodi??sasa iweje waje wakamate hawa wadogo huku mtaani?

3. Huyu jamaa anatumia umeme, na ananunua na kupata TRA risiti, sasa hiyo kodi anayokwepa ni ipi??

4. Kama lengo ni kulinda kazi za wasanii wa ndani....kwann hao wasanii wasilinde soko lao kwa kazi zenye ubora? Mtu anatunga fulamu kwa siku moja alafu anaingiza sikoni, kweli unataka ishindane na filamu iliyochukua miaka kutungwa tena na jopo la wataalam kwenye sekta hiyo achilia mbali teknolojia ya hali ya juu?

5. Sasa kama serikali haitoi hajira, sekta binafsi hazina ajira.... Bado watu wakijitaftia mia mbilimbili ili kuyamudu maisha bado mnawafanyia hivi ...je mnataka watu wafanyaje sasa......waingie msituni kupigania haki zao , maana nchi hii mnyonge ndo wakumwonea....

6. Au tuibe basi ili tuchomane moto mwenyewe kwa mwenyewe?

Inasikitisha sana .......nchi imekuwa ya uonevu, juzi watu wamepigwa na askari pale ukonga Mombasa leo anasimama kamanda wa polisi ana sema wale hawa kuwa polisi ...kweli jamani.....

Ila mi nnachojua hata mnyonge ukimwonea sana ipo siku atakufa ganz na kuamua kujitetea sasa.....maana wahenga walisema ngoma ikiwambwa sana hatimae hupasuka.....time will tell...

Asanteni...
 

sir mweli

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
495
1,000
Hii ndo selikal tuliyo ichagua mkuu bado miaka 8 tuvumilie
Hata kama....ila watambue kuwa na sisi ni binadamu na tuna moyo wa nyama....tuna milango yote ya fahamu ambayo kwa namna moja au nyingiane huhisi machungu....ipo siku yaja hatutakubali udhalimu huu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom