Huu niliofanyiwa sio utapeli?

Huu niliofanyiwa sio utapeli?

Freightliner

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
720
Reaction score
528
Siku moja wikiendi nilitembelewa na rafiki yangu hapa mjini Mbeya akitokea wilaya ya Mwakyembe huko tukakubaliana tukutane Kiwanja kimoja hapa mjini kinaitwa Mwailubi.

Lakini huyu rafiki alikuja na rafiki pia, tukakaa pale tukitupia moja baridi moja moto kifupi tulikuwa tunalipa kodi ya nchi. Huyu rafiki wa rafiki wangu ni mzuri sana basi nikaomba namba pale nikasepa kiutuuzima tukaanzisha mapenzi.

Kama unavyojua mapenzi lazima utagharamia na nilimgharamia hadi anavyoondoka kurudi kwa Mwakyembe. Alipokuwa kule pia ile mipigo kama kawaida hadi birthday ya mwanae ananambia kidume najitoa.

Juzi kati sasa kanambia nitumie nauli nije mjini, kidume nikatuma. Aisee alichofanya akaja mjini bila taarifa akanambia siko mjini kesho yake anasema niko mjini. Kumuuliza umekuja lini anasema ana siku kadhaa.

Nikamwambia haya basi tuonane akajibu ngoja nijiandae. Kidume najipa moyo hadi usiku unaingia kimya. Kumuuliza eti naumwa nitumie hela ya hospitali nikamwambia kesho.

Hiyo kesho ananambia karudi kwa Mwakyembe alizidiwa sana, hapa aliona atamtesa rafiki yake wa kufikia ila bado anataka nimpe hela.

Huu si utapeli huu?
 
badala ya kumpa izo ela mama yako, unampa malaya ?

jinga kabisa wewe
 
Huo sio utapeli ila ni zaid ya uchumi wa kati mkuu
 
Hili shauri lipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe kisha lipelekwe mahakamani maana mahakama ndiyo yenye uwezo kisheria kutafsiri sheria. Wao ndio watatuambia suala lako limekaa katika kundi gani la makosa!
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom