Tuna tatizo na thinking ya viongozi wetu. Busara ya kawaida kabisa ingewafanya hawa viongozi kukaa chini na kutafuta njia bura ya kutatua migogoro inayopamba moto sasa hivi nchini, hasa Mtwara. Lakini wameona wapande Treni na kwenda kusheherekea Kigoma!
Given hali halisi, massive unemployment, inflation, deni la taifa, wizi wa rasimali, njaa (zaidi ya Wilaya 20 zinakabiliwa na uhaba wa chakula), uhusioano mbaya kati ya Jeshi la polisi na rai, kuna haja kweli ya kusheherekea? Nadhani wakati mwingine CCM wanajitafutia kesi kwa kutofikiri sawasawa. Hata ndani ya familia, kama mambo hayaendi vizuri sherehe huwa zinaachwa pembeni.
Na jambo linalonishangaza ni ushiriki wa Dr Asha Rose Migiro kwenye haya mambo ya hovyo licha ya exposure aliyopata! Sasa hivi ni kama Tanzania iko kwenye auto-pilot. Kila kona wananchi wana hasira. CCM wanaona jambo la muhimu ni kusheherekea?