Huu ni uporaji au wizi

Huu ni uporaji au wizi

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,692
Reaction score
7,864

Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuachiliwa kwa sehemu ya kwanza ya mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa, akisema kuwa Iran itatumia fedha hizo kununua chakula kutoka kwa wakulima wa Marekani.

Abdolnaser Hemmati, mkuu wa Benki Kuu ya Iran, pia amethibitisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja taarifa hizo. Amesema kuwa dola bilioni 6 za kwanza zilizofunguliwa zitatumika kununua chakula na dawa kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Tehran na Washington mwaka 1402 kwa kalenda ya Iran.

Hemmati aliongeza kuwa dola bilioni 6 za pili, baada ya kuachiliwa, zitatumika kununua bidhaa ambazo hazijafungwa na vikwazo vya kimataifa.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, aliondoka kuelekea Muscat saa moja baada ya kurejea kutoka Uswisi.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa ni kwa ajili ya “maandalizi ya Iran ya usimamizi wa Mlango-Bahari wa Hormuz” pamoja na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili.

Aidha, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, anatarajiwa kufanya ziara nchini Pakistan katika siku zijazo kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia na kuimarisha mahusiano ya kikanda.

Kwa ujumla, hatua hizi zinaashiria kuendelea kwa mazungumzo na ushirikiano kati ya Iran, Marekani na nchi washirika wa eneo hilo, huku masuala ya uchumi, biashara na usalama wa njia ya bahari ya mlango bahari wa Hornuz yakipewa kipaumbele.
 
Hatua kubwa na ya kupongezwa! Hii inaonyesha kuwa diplomasia na mazungumzo daima ndiyo njia sahihi ya kutatua migogoro na kuleta utulivu wa kiuchumi duniani. Ni matumaini yetu kuwa ushirikiano huu utaleta tija zaidi kwa pande zote mbili. 🕊️✨
 
Hela yangu halafu unipangie matumizi?

Tena unipangie matumizi ninunue nini na nikanunue kwa nani?
 
Yaani wanakurudishia pesa zako halafu wanakulazimisha uzitumie kununua bidhaa zinazozalishwa kutoka kwao,kweli beberu sio mtu
 
Hatua kubwa na ya kupongezwa! Hii inaonyesha kuwa diplomasia na mazungumzo daima ndiyo njia sahihi ya kutatua migogoro na kuleta utulivu wa kiuchumi duniani. Ni matumaini yetu kuwa ushirikiano huu utaleta tija zaidi kwa pande zote mbili. 🕊️✨
Hapo diplomacy imechukua nafasi baada ya aliyekuwa anajiona ni mbabe kukutana na kisiki Cha mpingo , Aliyekuwa anajiona mbabe Kampiga mwenzie ngumi ya kifua yeye kapigwa ngumi ya pua na kuanza kutoka damu so akaona isije kuwa shida nikaumbuka zaidi ngoja nikimbilie diplomacy 😁
 
Mwisho wa siku, Donald Trump na viongozi wa Iran walipoona hakuna anayeweza kumsalimu amri mwenzake kirahisi, wakaona bora "wasafishe damu puani" na kukaa kwenye meza ya mazungumzo. Kufunguliwa kwa dola bilioni 6 za kwanza ili Iran wanunue chakula kutoka kwa wakulima wa Marekani ni dhihirisho tosha kuwa diplomasia ya sasa ni give-and-take (nipe nikupe) — Marekani inapata soko la mazao yake, na Iran inapata nafuu ya kifedha.
 
Yap pesa Ina Rudi USA ijapo kuwa USA haijaitoa Bure mpaka zilipochapwa 😄😄😄

Na watu wa Iran pia wanapata uhakika wa chakula

USA wamejikuta wana isafisha Iran na kuifanya igeuke kuwa almasi bila ya wao kupenda ila ndio hivyo wenye nguvu siku zote wanapaswa kuheshimiana
 
mzee unaongea ukweli mtupu! na vikwazo vya kipumbavu vya wazungu vimeifanya Iran kujitegemea na kuwa imara kama almasi. Mwisho wa siku, Marekani wamegundua kuwa ubabe wa kiuchumi una kikomo chake, na sasa wanalazimika kufanya biashara ili kulinda maslahi yao. Huu ni dhihirisho kuwa duniani wenye nguvu wakikutana, lazima waheshimiane kibiashara
 
Kabisa kabisa 🎯

Kuna Somo kubwa sana hapo limewekwa via Iran , kitakacho kufanya uwe salama na kuheshimika zaidi ni uwezo wako wa kujisimamia katika mambo Yako misimamo Yako kutokubali kuyumbushwa , Mbinu Bora za ubunifu katika utatuzi wa changamoto zako na Power
 
hakika mkuu
Katika mfumo wa hovyo wa hii dunia, tunajifunza kwa njia ngumu kwamba adabu na heshima hazitolewi eti kwa sababu wewe ni mwema sana au unaonewa; ila tunaona zinatolewa kwa sababu una uwezo wa kuleta maumivu au faida (wajomba zangu wagogo wanaita "Leverage"). sasa Iran walipojenga uwezo wa kijeshi na kiteknolojia unaoweza kutikisa usambazaji wa mafuta duniani na kulinda anga lao, walibadili mchezo. Kama huna "power" ya kuzuia adui asikuumize, diplomasia inakuwa ni amri ya mwenye nguvu kwenda kwa mnyonge.
 
Naam 📌 Absolutely

Mwisho umemalizia vyema sana
 
Waislamu wa Buza tumemaindi sana, kwanini wasizitumie kununua makobazi na tende kwa waislamu wenzao, wao wanazipeleka kwa makafiri kuwaungisha. Allah anafeli wapi sijui.
 
Back
Top Bottom