Huu ni ukweli kamili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni ukweli kamili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jul 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Marehemu Hekima Bakari.

  Marehemu Fikiri.
  [​IMG]
  Marehemu Banzi.Jeneza lenye mwili wa marehemu Banzi.

  Na Haruni Sanchawa

  UKWELI kamili kuhusu vifo vya watu sita waliokunywa gongo Kigogo Sambusa Luhanga Darajani, ambapo wengine wamelazwa wakiwa hoi katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam umebainika.

  Gazeti hili limegundua kuwa gongo waliyokunywa ilikuwa ina mchanganyiko wa kemikali mbalimbali na dawa za viwandani na tayari sampuli yake imepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

  Mteja mmoja ambaye kwa kipindi cha nyuma alikuwa ‘mnywaji mzuri’ wa gongo katika eneo hilo ambaye hakutaka atajwe gazetini alichambua jinsi pombe hiyo inavyotengenezwa.

  Alisema kuwa kuna kemikali zinozotumika kutengezea konyagi ambapo watengenezaji wanazipata katika kiwanda kimoja (jina tunahifadhi) na wanachanganya na dawa nyingine.

  Alibainisha kuwa kemikali moja hujazwa kwenye chupa ya ujazo wa lita moja na kuchanganywa na maji kiasi cha lita kumi kisha hutiwa spiriti pamoja na dawa ya madoa iitwayo ‘jick’ na mchanganyiko huo huzalisha kitu kinachoitwa gongo na kuanza kusambaziwa wateja.
  Chanzo hicho kilisema kuwa njia hiyo ndiyo aliyokuwa akiitumia Hekima Bakari kwa muda mrefu, mama anayedaiwa kuwauzia gongo watu waliofariki na kulazwa Hospitali ya Amana.
  Kiliendelelea kufafanua kuwa mama huyo ametengeneza mtandao na alikuwa akisambaza kinywaji hicho Gongo la Mboto, Kipunguni, Chanika, Kitunda, Kimara Bucha na Kigamboni.

  Gongo hiyo ilianza kuua Jumatatu ya wiki iliyopita ambapo ilimuua Juma Abdallah baada ya kunywa kinywaji hicho na wanywaji wengine wakawa wanajificha kwa kuwa walikuwa wakiogopa kukamatwa na polisi.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa katika eneo hilo la Kigogo Mbuyuni, Mohammed Mnunga aliwataka wote waliokunywa gongo hiyo kujitokeza na kwenda kupimwa afya zao kwa usalama wao.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amepiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na kupika, kuuza au kunywa pombe haramu ya gongo na akasema tayari watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na sakata hilo.

  Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kuwa ni Ramadhan Selestin (30), Salehe Omary (17), Shukuru Marungu (20), Charles Ibrahim (20), Fadhili Juma (20) wote ni wakazi wa Kigogo na Abdallah Mnazi (30) mkazi wa Tabata.

  Aliwataja pia waliofariki katika nyakati tofauti kuanzia Julai 7 hadi 12, mwaka huu, katika maeneo ya Kigogo Mbuyuni kuwa ni Juma Abdallah (60), Mathew Roman (35), Khalid Hamis (31), Mohamed Said (25) na Antipal Raphel (60) wote wa Kigogo Mbuyuni na Hekima Bakari, ambaye ni muuzaji wa gongo hiyo.

  ​HUU NI UKWELI KAMILI - Global Publishers

 2. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UKWELI kamili kuhusu vifo vya watu sita waliokunywa gongo Kigogo Sambusa Luhanga Darajani, ambapo wengine wamelazwa wakiwa hoi katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam umebainika.
  Gazeti hili limegundua kuwa gongo waliyokunywa ilikuwa ina mchanganyiko wa kemikali mbalimbali na dawa za viwandani na tayari sampuli yake imepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
  Mteja mmoja ambaye kwa kipindi cha nyuma alikuwa ‘mnywaji mzuri’ wa gongo katika eneo hilo ambaye hakutaka atajwe gazetini alichambua jinsi pombe hiyo inavyotengenezwa.
  Alisema kuwa kuna kemikali zinozotumika kutengezea konyagi ambapo watengenezaji wanazipata katika kiwanda kimoja (jina tunahifadhi) na wanachanganya na dawa nyingine.
  Alibainisha kuwa kemikali moja hujazwa kwenye chupa ya ujazo wa lita moja na kuchanganywa na maji kiasi cha lita kumi kisha hutiwa spiriti pamoja na dawa ya madoa iitwayo ‘jick’ na mchanganyiko huo huzalisha kitu kinachoitwa gongo na kuanza kusambaziwa wateja.
  Chanzo hicho kilisema kuwa njia hiyo ndiyo aliyokuwa akiitumia Hekima Bakari kwa muda mrefu, mama anayedaiwa kuwauzia gongo watu waliofariki na kulazwa Hospitali ya Amana.
  Kiliendelelea kufafanua kuwa mama huyo ametengeneza mtandao na alikuwa akisambaza kinywaji hicho Gongo la Mboto, Kipunguni, Chanika, Kitunda, Kimara Bucha na Kigamboni.
  Gongo hiyo ilianza kuua Jumatatu ya wiki iliyopita ambapo ilimuua Juma Abdallah baada ya kunywa kinywaji hicho na wanywaji wengine wakawa wanajificha kwa kuwa walikuwa wakiogopa kukamatwa na polisi.
  Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa katika eneo hilo la Kigogo Mbuyuni, Mohammed Mnunga aliwataka wote waliokunywa gongo hiyo kujitokeza na kwenda kupimwa afya zao kwa usalama wao.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amepiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na kupika, kuuza au kunywa pombe haramu ya gongo na akasema tayari watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na sakata hilo.

  KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: HUU NI UKWELI KAMILI KUHUSU SAKATA LA WALIOKUFA KWA KUNYWA GONGO
   
 3. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  hakuna ukweli kamili wakati majina ya kampuni na kemikali zilizotumika hamzitaji.
   
 4. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Kwani hii tunaruhusiwa kujadili pia ,kwani haiko mahakamani?!watu wengi wamekufa bado mnajadili .Kweli inahitaji muda niweze kuielewa Tanzania
   
Loading...