Huu ni ujumbe kwa Wasanii wote wa mziki, Diamond hafai kuweni naye makini

timu yko ishajulkana uzi wa kishabiki kabsa....me ofcoz cmkubali kbs diamond ila napenda baadh ya nyimbo zke...dogo anajituma sn lkn wasanii wenzake mara nying ndo uwa wanaanza kumchokonoa chokonoa....alikua anakaa kimya ila hili la dimpoz ikabd alijibu kwa kupanic na matuc.....apo alikosea sn na alinkera sn kujibishana
 
Tatizo akina Kiba ni walalamishi sana hata kama hawajaonewa.
Kama ni promo vituo vyetu vya redio/television havibagui
Wapige kazi nzuri ( nyimbo nzuri + videos).. Kisha promo ya ukweli

Badala ya kuwatumia akina Shilolekiuno kutukana wawatumie kujenga fan base kubwa.
Wafanye collabo na wasanii wakali kwa muda husika ( Kama Mond alivyofanya No.1 remix )...
Mziki mzuri ndo umemtoa Tekno tena bila collabo...
 
Kuna kitu kinaitwa Muziki by darassa ft Ben Pol, yaaani kwa jins ngoma ilivyo kali na haihit kiviiileee ndo huwa naamini huenda figisu + ushirikina ndo vinaitawala industry nowadays
 
Mi ushabiki na hawa watu najitahidigi ila nashindwa bora niwe shabika wa braza Trump
 
Inabidi tuwe nae makini kwasababu anasaidia vijana wenzake.
Kaajiri vijana zaidi ya 20,katoa vijana wawili waliokua mtaani . Leo hii wanaiwakilisha nchi vizuri sana.
Inabidi uyu kijana tuwe nae makini ili aendelee kusaidia vijana wengine zaidi.
 
watu wanaojifanya huu mziki ni wakwao na wakawapa viburi baadhi ya wasanii walio kwenye imaya zao ndio wanaotusumbua,Dimond hajamtoa yeyote hapa bongo na wala asipate kiburi bila hao wanamfanya ajishembendue kusengekua na WCB na kujisifu amewatoa wasanii.
Tukumbushane THT iliyokua na wasanii wengi lakini mwenye kipaji cha uhakika ni Barnaba peke wengine wote walikua wazugaji tu,kila aliyepiga nyimbo na Barnaba alivuma akiwemo Amin,Linah na Pipi, leo wakowapi....Kumbe THT ya wanaojifanya huu mziki ni wakwao ndo iliwatoa na ilikua ikiwabeba nA SIO BARNABA..kwa hiyo Mond asivimbe kichwa mziki wa bongo na harakati zake tunazijua vizuri.
Umetokwa povu,kisha umeongea upuuzi mtupu.
 
Mleta mada ndugu utandu , ni lini na wapi umewahi kuona Diamond akimchokoza msanii yeyote yule? Kwa nini Diamond akijibu chokochoko anazofanyiwa na akina Alikiba, Dimpoz na wengine mnaomuona Diamond ndiyo mwanzilishi? WCB walitoa wimbo wao na wakawa wanaupromote kama wanavyofanya nyimbo nyingine, huku na huku Dimpoz kaanza mipasho, je mlitaka Diamond akae kimya? Huyo huyo Dimpoz kalike post yenye matusi ya nguoni aliyotukanwa Diamond na familia yake, je mlitaka Diamond akae kimya ndipo nafsi zenu zilidhike? Au Diamond yeye ni chuma hapatwi na maumivu anapotukanwa? Watanzania tuache unafiki. Hakuna siku hata moja ambayo Diamond amewahi kumchokoza Alikiba wala Dimpoz, siku zote Diamond hujibu visa vinavyoanzishwa na hao mnaowatetea.
 
Kwanza niweke wazi miye sipo timu yoyote ile ila ni mdau wa huu mziki tangu unaanza kukubalika nimekuwa mdau kabla

Prof Jay ajatoka
Gangwe mob, juma nature hawajatoka

Mda mabaga fresh wapo hot nature ajulikani

Enzi za mama mwenye nyumba nk

Sogy dog dog hunter, CAZ T wanasumbua walk man zetu

nk kwaiyo kidogo historia ya mziki huu tangu uanze kulipa naijuia

Sasa nachotaka kusema nini diamond ni msanii mzuri, ana uwezo mzuri sana ila tatizo moja Kijana hajiamini anataka yeye awe yeye tu hilo ndio tatizo lake yeye na uongozi wao hawataki kubali changamoto ambazo ndio zilizowezesha diamond akatoka kimuziki endapo wasanii waliotangulia wangekuwa na roho ya husda kama yake diamond asingetoka

Diamond na uongozi wake hawataki kuona msanii mpya au wazamani anachukua nafasi ya kimuziki yani msanii asikike kazi zake hii ipo wazi kabisa

Kwaiyo wasanii mnatoa nyimbo angalieni hilo suala katika promo zenu msije kuta nyimbo zenu nzuri ila zinafanyiwa figisu ili zisitambe kwa lengo moja tu nyimbo nzuri zikiwa nyingi basi upo uwezekano jamii ikamzoea diamond nikaona kawaida tu hivyo juhudi zimekuwepo kuhakikisha nyimbo nzuri za wasanii wengine hazipati nafasi ili diamond akiachia wimbo usumbue hii ipo wazi

Na hii nimebaini baada ya huu ugovi wa hawa watu diamond na omy dimpoz yani baada ya dimpoz na kiba kuachia wimbo nyie mmeona kama diamond alipanic hivi kaachia nyimbo kwa fujo

Kaenda media kaongea vitu vya ajabu kwa level yake kimuziki ili budi astilli maneno ila Kijana kapanic

Hivyo wasanii angalieni huyu Kijana si mzuri kabisa

Fikilia hizo tabia angekuwa nazo

Dully
Prof
Nk
Je wasanii kama kina diamond wangesikika

Ni mtazamo tu yani kuwa na tabia ya wao kutaka kuwa wao tu
Unachuki binafsi
Utamzuiaje Judith wambura,AY,Mwana FA wasitambe?
Ukweli ni kazi nzuri ndio humfanya msanii atambe
Watu wa Kiba acheni kulia lia
 
Ktk maisha hamna kitu kizuri kama kujiamini, diamond platnumz anajiamini maadui Zake hawajiamini, ndio maana kila siku wanataka kuonewa huruma, wanataka kubebwa kupitia diamond platnumz na ndio maana hawaishi kulalamika. Nawaonea huruma vijana wa tz kama mnafikiri kama huyu aliyepost huu uzi. Acha kuzunguka ooh mimi sina timu yoyote wakati, unachokiandika kina reflect upo timu kiba. ACHA KUZUNGUKA KAMA DAWA MBU YA KUCHOMA, KAMA MTU HUMPENDI SEMA SIMPENDI na sikuanza kumpakazia ubaya aonekane hafai, kwa tz hamna msanii aliyetoa ajira kama diamond platnumz, ana watu zaidi ya 30 kawa ajiri, anawabeba kuanzia wao na familia zao, amewabeba harmonize na rayvany from zero mpaka sasa wanapata nomination ktk tuzo na kolabo za kimataifa. Wabongo tubadilike tuwatie moyo watu wanaofanya vizuri, sio kuwajengea chuki na majungu.
 
Umezunguka kote ila nimeona hata wewe una timu...kila binadam ana hasra...kutukanwa na kuvumilia ni shida kwa watanzania...dai nae ni binadamu...kwani mangapi kasemwa Hutu chalii but mbona hukuwazungumzia...leo dai katoa kajibu lishakuwa gumzo...usiamin upande mmoja mkuu...nenda kamuulize dai kama ndo utajaji vizur...huyo ommy na wenzie wamewasaidia wasanii gani hapa bongo..acha husuda mkuu...bora wazir akataze kuchat mida ya asubui na mchana ili muache kuanzisha thread chonganishi ...!!
 
Hizo kelele tu ukitaka umjue mtu angalia washkaji zake diamond washkaji zake ni wakina Kikwete Makonda Jpm na wengine wazito kama hao sasa hao unaowasifia tumchukue kiba washkaji zake ndio hao wakina mziwanda wema hilo lakwanza jingine ni kuwa hivi dai ni nani wakuzuia wimbo usipigwe kwenye media waulize watu waliofanikiwa kwenye mziki kama AY watakwambia dai ni mtu wa aina gani
 
mhh! mtu ambaye:-
1. kawatoa wasani wawili mavumbini hadi kuwa mastaa wakubwa kuliko baadh ya waliokaa kwenye game miaka kumi na ushee...

2. ameajiri vijana si chini ya thelathini na kuwalipa mishahara kiasi cha kujenga na kumilika usafiri...

3. ameweza kuleta mapinduzi ya mziki kuwa biashara (kuongeza thaman ya msanii)

4.. N.K


HAYA NGOJA TUWE MAKINI NAYE BASI MKUU
Sorry, mimi SIPO TIMU YYT ya muziki, ila ni shabiki wa timu ya Arsenal.

Naomba kutofautiana na wewe hapo kwenye namba 2. Kuajiri watu ni jambo moja, na kununua hayo magari na kujenga ni jambo jingine.

Lazima ufahamu kwmb na yeye anafaidika sn na kuwa na hao vijana. Mimi na wewe HATUJUI NI KIASI GANI WANANYONYWA.

Ni watumishi wangapi wameajiriwa na wana magari na nyumba, but they are still complaining..???

Wat if jamaa akawa anawakandamiza na hataki wawe ma-star kma yeye cz anaamin watamfunika ila anachofanya ni kuwahakikishia wanakuwa smart ili kumaintain jina la WASAFI. Who knows??

Kwa mtu anayeingia mkataba wa billions of money, wat is gari na nyumba bana..!!

Nadhani ni ndoto ya kila upcoming artist, nyimbo yke kupigwa CLOUDS. Sijui, bali nadhani pia Clouds na Diamond ni damu damu. Wat if ukazingua kwake WCB, halafu akaziba nyimbo zako kupigwa clouds?? Hudhani labda wapo wanaotamani kutoka ila wanaogopa kitu kma hicho??

Binafsi kinachoniboa kwa wale watoto ni kujaribu kumuiga Diamond kila kitu, hasa yule Rayvan. Kuanzia jinsi ya kucheza mpka wanavyobetua mdomo. Nadhan angetoka kivyake vyake ingependeza zaidi.

Ni hayo tu.
 
Sijui mi uzee, hata sipendi hizo nyimbo. Na hata huu uzi umefunguka kwa bahati mbaya sana
 
Huyo Kijana ni hatari Sana amekuwa akinunua tuzo ikapelekea wasanii wengine kukata tamaa na wengine kufa kwa madawa wakitaka kushindana nae. Alert ulioitowa wenye akiri ndo wataielewa. Jamaa yupo tayari kupambana ili wenzie wasitoke. Kawachukuwa kina rayvan ili wamsitili maana kwa sasa hana kipya katika gem.
 
Back
Top Bottom