Huu ni ujinga mkubwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni ujinga mkubwa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bendera ya bati, Jul 5, 2011.

 1. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiingia katika migogoro ya hapa na pale na vijana kama tulivyozoea kuwaita "makonda"wa mabasi yanayofanya trip zake kati ya Mwenge-Bunju hapa katika jiji la Dar es Salaam.Kikubwa kinachonifanya kukorofishana nao hawa vijana wenzangu na hata abiria wenzangu wakibaki kunishangaa,ni pale wanapoleta mchezo mchafu kwa abiria wa kukatisha route,mfano wakiwa mwenge utasikia wanapiga debe kuwa route yao inaishia Tegeta,lakini ikumbukwe kwamba gari lenyewe limesajili kufanya route za mwenge na Bunju.

  Chakushangaza sasa,utaona watu wanaibiwa hivi hivi wala hawahoji sababu za kushushwa tegeta ili hali gari limesajiliwa kufanya ruti za mwenge na bunju.sasa huu si ujinga.....mimi siku zote nimekuwa nikikomaa na makondakta mpaka nifikishwe kituo changu cha kushuka hadi hivi sasa wamenizoea.
  Sasa nimekuwa najiuliza maswali haya yafuatayo kuhusu tatizo hili ;
  1.Je?sisi wtz especially tunaotumia usafiri huu tuna hela sana kiasi kwamba hakuna haja yakujisumbua kuhoji.
  2.Watz ni watu wakuburuzwa tu hata kama wanajua kipi ni haki na kipi si haki kwao hata kama wanaviwango vya elimu ya juu?
  3.Au ile 'spirit' yetu ya Watz ni watu wa amani,ndicho chanzo cha kuporomoka kwa confindence hata tusijue kupigania haki zinazostahiki?
  4.Au uoga wetu ndio hasa source ya kuonewa?
  Wadau hebu nisaidieni tatizo hapa ni nini????NAOMBA KUWASILISHA.
   
Loading...