SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,280
Unamwona mtu anafanya kitendo ambacho unajua kabisa matokeo yake ni mabaya sana
kwake, unamshauri aache lakini unakuona wewe ni zoba.
Muda si mrefu mabaya kweli yanamtokea na anatembea mtaa wote kukusema kwamba wewe
una 'mdomo mbaya'. Watu wasiojua matokeo ya matendo yao au ya watoto wao ni hatari sana.
Juzi juzi kama mwezi wa tano hivi, kuna watoto mtaani kwangu walikuwa na tabia ya kufukuza/kukimbia nyuma ya
kila gari linalopita na wakati mwingine kusimama kwenye bumper la nyuma na kupata 'free ride'.
Kwa kuwa nawafahamu baadhi ya hao watoto, niliwaona wazazi wao na kuwaomba wawakanye hao watoto
waache hiyo tabia ya kudandia magari kwa nyuma kwani ni hatari sana.Hakuna hata mzazi mmoja aliyejigusa.Kinyume chake mzazi mmoja (mama) alidiriki kuniuliza kama hayo magari yanayodandiwa ni yangu.'Wenye magari wamekaa kimya wewe kinachokuwasha nini?' aliniuliza huyo mama.
Mie nikajinyamazia.Mwezi wa sita na saba ukaisha.Mwezi ulioisha ukiwa katikati, ikapita gari aina ya noah na watoto watatu haooo kama kawaida wakaifukuza kwa nyuma.Mmoja akapanda kwenye bumper la nyuma.Mwenzake mmoja akaona anapitwa, akamvuta yule aliyepanda ili achukue nafasi yake.
Aliyevutwa alidondoka chini uso ukagonga kwenye udongo barabarani (barabara si ya lami)
Huyo mtoto aliumia sana usoni na mama yake ndo yule mbishi.
Sasa hivi huku mtaani naitwa mchawi mwenye mdomo nuksi ninayewatakia watoto mabaya!
Sijui watu wengine wakoje!!!!