Huu ni ugonjwa gani kwa kuku?

namba force

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
758
434
Wadau habarini za mchana huu! Mwenzenu nina ufugaji wa Kuku wa asili na Mungu kanisaidia wamefika 300 na ninatumia mfumo wa zero grazing.

Kuna huu ugonjwa Kuku kama 10 yote majogoo miguu inakosa nguvu na kushindwa kutembea. Nimeuliza wataalamu wa Maduka ya madawa ya mifugo nao wanashangaa tu.

Naomba wajuvi mnisaidie.
 
Wamekosa madini muhimu mwilini kama calcium ambayo hupatikana kwenye dagaa, konokono au uduvi, hakikisha chakula chao unachanganya DCP, mifupa na chokaa.

Kwa kuwaokoa na wengine kwa haraka tumia DCP kwenye maji ya kunywa na nyingine changanya kwenye chakula kwa uwiano ulio sahihi, usichakachue au simamia mwenyewe usimpe mtu kuandaa chakula ukiwa haupo.
 
Changanya maji chumvi ya mabonge wanyweshe na mengine wamwagie miguuni
 
Angalia Uzito wao inaweza kuwa ni sababu, pia je wana sehemu ya kutosha kufanyia mazoezi yaani kuzungula zunguka? Pia angalia calcium
 
Pole sana najua ujaenda maduka ya mifugo ila huo siyo ugonjwa ni condition tu imawepata ambapo chakula unachowapa kina upungufu wa madini ya calcium na phosphorus
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom