aliyetegwa
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 312
- 483
Habarini wana jukwaa, ama baada ya Salam ningependa kuwashirikisha kinachoufukuta moyo wangu ikiwa ni mara yangu ya kwanza kabisa kwani mara zote nimekua msomaji mzuri na mchangiaji tuu.
Mtanisamehe maana si mwandishi mzuri hivyo mtiririko wa habari unaweza kua si mzuri pia.
Ni habari ya kweli ni tukio lililotokea jana na nikabahatika kushirikishwa, katika hali isiyo eleweka jana mtoto mdogo wa miaka nane alikutwa nguo zake zikiwa zimechafuka kwa damu ambayo ni mbichi kabisa ama baada ya kumkagua akagundulika damu hizo zilikua zikivujakota katika sehemu zake za siri pia nguo yake ya ndani ilikua imejaa kinyesi, baada ya mtoto kuulizwa amepatwa na nini alitaja jina la kaka yake ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa kabisa mwenye umri wa miaka 28 kua ndo aliyemuumiza,
Ilisababisha taharuki ya aina yake maana watu hawakuweza kuamini icho kitu kwa uraisi, uyo kaka alitafutwa na kupewa tuhuma zilizopo lakini alikataa kata kata kua hajausika na wala hakua umeonekana katika maeneo ambayo mtoto uyo anaishi(ikumbukwe kwamba mtoto anaishi katika kijiji tofauti na kile anachoishi kaka)
Mungu saidia za mwizi arobani kumbe kuna watu walimuona pale kijijini na maeneo ya kwao na mtoto akiwa ikizengea zengea, wakasema mbona tulikuona ukiwa umevaa suruali nyeupe na shati jeusi akaishiwa nguvu maana mpaka mda ule alikua amevaa ivyo ivyo, wanandugu wakajiridhisha moja kwa moja kwamba kaka mtu ndo alihusika katika unyama ule dhidi ya mtoto ambaye ni mdogo wake wa damu.
Ikabidi mtoto aulizwe vizuri na kusema hiyo siku haikua siku ya kwanza kufanyiwa unyama huo, amekua akifanyiwa mara kwa mara. Kilichonisikitisha ni watu hao kuamua kulimaliza ili jambo la kiuwaji lililojaa kila aina ya unyama kindugu kwa kuamua kaka mtu apate adhabu ya viboko kutokana na kosa ilo kwa kuhofia kama litapelekwa mbele kisheria kaka mtu angefungwa na familia haiko tayari kwa hilo.
Nimeumia sana kufikia atua ya kulia maana adhabu hiyo ni ndogo mno kwa mtu aliyetenda kosa la kiuaji kiasi icho kwa mtoto mdogo asiyejua chochote ambaye ndiye kiongozi na taifa la kesho.
HISTORIA YA FAMILIA YA MTOTO.
Baba na mama wa mtoto waliachana kitu kilichopelekea mama kuondoka na kuwaacha watoto kwa baba yao, watoto wamekua wakikaa bila uangalizi maalumu maana baba hundoka asubuhi kwenda kwenye mihangaiko na kurudi kuwachungulia kidogo jioni kisha huondoka tena na kurudi asubuhi akitokea kwenye kazi yake ya ulinzi.
Baadaye baba aliamua kuoa binti mdogo wa miaka 20's ilihali yeye yupo kwenye 50's baada ya kuoa hakutaka kukaa na mtoto hivyo alimchukua na kumpeleka kwa dada yake(shangazi wa mtoto) ambako ndiko alikokutwa na majanga hayo.
Wito wangu kwa akina mama.
Haijalishi unapitia magumu gani katika familia yako lakini katu usije kuondoka ukaacha watoto tena ambao ni wadogo maana mwangali na mlezi wa watoto ni mama wakina baba hawawezi, pigana mpaka pumzi yako ya mwisho kuhakikisha watoto wako wanapata malezi bora na wanakua salama, ikishindikana ondoka nao lakini usiache watoto nyuma.
Natamani kama kitu hiki kingeweza kifika katika sheria ili adhabu sitaiki itolewe lakini napata wakati mgumu nafanyaje wakati familia imeamua kuyamaliza kindugu??
Nipeni ushari nini kifanyike ili kuweza kuweka unyama huu hadharani maana kuendelea kuuficha ni kundeleza kuitekeza jamii yetu changa na kuendeleza mmomonyoko wa maadili.
Natanguliza shukurani, poleni kwa maandishi marefu ila mchango wenu ni mhimu.