Huu ni mwanzo wa watumishi wa umma kuvunjika moyo

mgoli magombe

Senior Member
Apr 20, 2013
121
27
Inashangaza sana kuona kuna watu katika utumishi wa umma ambao ni Maafisa Tawala, wengine ni Maafisa Tarafa, wengine ni Makatibu Tawala wasaidizi mikoani wakibaki bila kujua vyeo vyao kimuundo vitakuwaje.

Na je wakifanyiwa promotion wanakuwa kina nani? Maana nafasi walizokuwa wanatakiwa wapandishwe ndo wamepewa watu ambao hawana hata uzoefu kisa ni makada. Kitakachofanyika kazi hazitofanyika kwa moyo maana kuna watumishi kama maafisa tarafa pikipiki zao serikali haiwawekei hata mafuta lakini wanaweka wao na kazi zinaendelea

Kweli politics is the only game in town.
 
serilali ilashaona mtumishi ndo mtu mnyonge dunia nzima
 
inashangaza Sana kuona kuna watu katika utumishi Wa umma ni maafisa tawala, wengine ni maafisa tarafa, wengine ni makatibu tawala wasaidizi mikoani wakibaki Bila kujua vyeo vyao kimuundo vitakuaje?. na je wakifanyiwa promotion wanakuwa kinanani? Maana nafasi walizokuwa wanatakiwa wapandishwe ndo wamepewa watu ambao hawana hata uzoefu kisa ni makada. kitakacho fanyika kazi hazito fanyika kwa moyo Maana kuna watumishi Kama maafisa tarafa pikipiki zao serikali haiwawekei hata mafuta lkn wanaweka wao na kazi zinaendelea. kweli politics is the only game in town.
Mbona na wao inabidi wabadilishwe?
 
Nafasi zao zimejazwa na ajira mpya makada wenzetu hakuna shida. Japo sikupenda kuingizwa kwa siasa katika utendaji. Wangebaki kukiimarisha Chama watumishi wa umma waendelee kupiga kazi. Lakini ndio hivyo hawaaminiwi na wanasiasa. Athari zake ni kuingizwa kwa shughuli za siasa katika utendaji.
 
Hili la kuteua makada wa CCM kuwa maDAS na maDED ni tatizo kubwa. Yaani kuanzia RC mpaka katibu kata wote makada nambari one. Very soon tutahamia kwa RWEs, RMOs, RHOs, DWEs etc etc. Yaani technocrat posts zote weka makada nambari one ili ilani ya nambari one ikafanyiwe majaribio ya kutekelezwa. We are doomed.
 
Ngoja tuone wanamnufaisha nani chama au mwananchi ? 2020 tutapata sababu....
 
Inashangaza sana kuona kuna watu katika utumishi wa umma ambao ni Maafisa Tawala, wengine ni Maafisa Tarafa, wengine ni Makatibu Tawala wasaidizi mikoani wakibaki bila kujua vyeo vyao kimuundo vitakuwaje.

Na je wakifanyiwa promotion wanakuwa kina nani? Maana nafasi walizokuwa wanatakiwa wapandishwe ndo wamepewa watu ambao hawana hata uzoefu kisa ni makada. Kitakachofanyika kazi hazitofanyika kwa moyo maana kuna watumishi kama maafisa tarafa pikipiki zao serikali haiwawekei hata mafuta lakini wanaweka wao na kazi zinaendelea

Kweli politics is the only game in town.
Shangilia si mmezoea
 
kuna chalii nilikuwa nae chuo then akachemsha njiani tukamuacha akarudi kitaa akapiga siasa sasa hivi ameula sasa hivi kawa katibu tawala duh kweli siasa woyeeee
 
Inashangaza sana kuona kuna watu katika utumishi wa umma ambao ni Maafisa Tawala, wengine ni Maafisa Tarafa, wengine ni Makatibu Tawala wasaidizi mikoani wakibaki bila kujua vyeo vyao kimuundo vitakuwaje.

Na je wakifanyiwa promotion wanakuwa kina nani? Maana nafasi walizokuwa wanatakiwa wapandishwe ndo wamepewa watu ambao hawana hata uzoefu kisa ni makada. Kitakachofanyika kazi hazitofanyika kwa moyo maana kuna watumishi kama maafisa tarafa pikipiki zao serikali haiwawekei hata mafuta lakini wanaweka wao na kazi zinaendelea

Kweli politics is the only game in town.

Mwaka jana (2015) mwezi wa nne nilikwenda msibani maeneo ya Busokelo Rungwe. Katika maongezi pale msibani, viongozi wakuu wa idara za halmashauri mpya ya Busokelo ndiyo walikuwa wapiga debe wakubwa wa Ukawa. Wenyewe walikuwa wanaita kumwaga sumu. Na naamini hata mtendaji mkuu wa halmashauri naye alikuwa pande hizo (japo sina uhakika sana kwa hili). Watendaji wengi walilishwa sumu wakaingiza siasa waziwazi. Matarajio yao yamefeli ndio maana wanalalamika. They backed the wrong horse! Ukaskazini na culture ya malalamiko na kulaumu ilikuwa imewajenga upofu watendaji wengi.
Unamsikia mkuu wa idara (ambaye yuko kwenye duka lake la pembejeo la vifaa vya kilimo saa 3 asubuhi badala ya kuwa ofisini au kwenye shughuli za field) analalamika jinsi serikali ile inavyoshindwa kufanya kazi, bila kutambua kwamba yeye ni extension na part ya hiyo serikali. Ubunifu zero, utendaji zero, wamekalia kuzungumzia idadi ya vyeti walivyonavyo, na siyo kuutumia ujuzi walio nao kutatua matatizo ya wananchi na kuleta ufumbuzi wa changamoto zinazoukabili umma wa watanzania.

Wengi walikuwa wanasubiria posho za semina na vikao, na madeal ya ujanja ujanja tu. Ndiyo maana hivi sasa wanalalamika kama watoto, kwa kuwa wakifanya yote hayo (kuleta siasa katika utendaji) walidhani wenzao hawaoni. UKAWA NDIYO WALIOANZA KUPELEKA SIASA KWA WATENDAJI, MAGUFULI ANAKAMILISHA TU. ILA YEYE SIYO MNAFIKI ANAFANYA MCHANA JUA LINAWAKA.

Kama ni kumshauri, Mheshimiwa Rais; asijibishane na mpumbavu yoyote aendelee kwa namna alivyoanza, namna itakayomuhakikishia accountability. Hao waliowekwa wanauwezo wa kuwathibiti walio chini yao; anayeleta dharau au kukwamishwa apishe tuwaletee watanzania maendeleo ya kweli.

NB: Mimi siyo mfanyakazi, na pia si mwanachama wa chama chochote. Ni mkulima, mchuuzi mdogo mdogo, na mfugaji.
 
Tuliambiwa CCM imepoteza uwezo wa kuwalipa mishahara watumishi wao!!

Sasa kodi zetu zinawalipa mishahara kwa mgongo wa nyuma! Tunaisoma ......!!!
 
Back
Top Bottom