Salaam! Nina mdogo wangu wa kiume, alikuwa mbaya(sura mbaya) tangu utoto wake, mademu wengi walimkataa sana.
Mwaka 2019 alijiunga na chuo nako bado alikataliwa kwa dharau sana. Ikapita miaka 2 yaani mpaka mwaka huu, amerudi likizo nashagaa, yaani wotr tumemshangaa sana, kawa handsome balaa, ameota tundevu na uso wake umebadilika.
Yaani kichwa kimekuwa kirefu chenye mvuto kifupi mpaka mwenyewe nimeshangaa sana, na ameanza kuwapanga mademu vibaya mno.
Kwa wajuaji, hivi kuna mabadiliko yoyote ya mwili wa binadamu kwa miaka 2, hususani sura na kichwa kwa kijana wa miaka 21? Kwa sasa ana miaka 23. Nimeshangaa mno kilichomtokea huyu dogo.
Nawasilisha!