Huu ndiyo mtizamo wa Magufuli kuhusu demokrasia na siasa. JE, yuko sahihi?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..Je, hayo anayoyasema hapo ndiyo uhalisia wa mambo?

..Je, ni kweli Maraisi wastaafu wa Marekani huwa hawamkosoi Raisi aliyeko madarakani?

..Je, Raisi aliyeko madarakani hapaswi kukosolewa na watangulizi wake?

..Je, ni kweli kwamba vyama tawala huwa havikosolewi, isipokuwa wakati wa uchaguzi? kwamba huachwa "viboronge" au vipatie na huja kuulizwa wakati wa uchaguzi tu?

..Je, ni kweli kwamba hapa Tanzania kilichokuwa kinaendelea ni MATUSI na siyo siasa za ushindani zinazoshabihisha hoja za wananchi?

..Kama kulikuwa na MATUSI, je suluhisho lilikuwa ni kufungia mikutano ya hadhara?

 
Kuhusu Marekani na marais wake wastaafu, yupo sahihi kiasi na kakosea kiasi.

Kwa muda mrefu ulikuwepo utamaduni wa marais wastaafu kutokumkosoa rais aliyepo madarakani.

Ila kama sijakosea, utamaduni huo ulikuja kuvunjwa na Bill Clinton.

W. Bush hakumkosoa Obama, nadhani.

Obama anamkosoa Trump.

Pia sikumbuki Reagan kumkosoa George H. W. Bush.
 
Kuhusu Marekani na marais wake wastaafu, yupo sahihi kiasi na kakosea kiasi.

Kwa muda mrefu ulikuwepo utamaduni wa marais wastaafu kutokumkosoa rais aliyepo madarakani.

Ila kama sijakosea, utamaduni huo ulikuja kuvunjwa na Bill Clinton.

W. Bush hakumkosoa Obama, nadhani.

Obama anamkosoa Trump.

Pia sikumbuki Reagan kumkosoa George H. W. Bush.


..JE, huko Marekani uchaguzi mkuu ukiisha mikutano ya kisiasa nayo hufungwa mpaka uchaguzi mwingine?

..JE, Raisi aliyeko madarakani[ amemtaja Donald Trump] huwa hakosolewi mpaka wakati wa kampeni za uchaguzi?
 
..Je, hayo anayoyasema hapo ndiyo uhalisia wa mambo?.
Mkuu Joka Kuu, yes, aliyoyasema ndio uhalisia wa mambo na ndio ukweli wenyewe, kwa sababu ameanza kwa kueleza wazi, kila nchi na siasa zake, tena sio siasa tuu, bali kila nchi na demokrasia yake, huwezi kutumia democracy model ya Marekani na kuifit Africa, kinachafonyika ndio Tanzanian model of democracy na ndio demokrasia yetu. Na kila zama na zama zake, Mkapa na JK, waliteua wapinzani Bungeni, Magufuli alisema hateui mpinzani, ila amewateua u RC, hadi PS!. Siasa wakati wa JK zilikuwa siasa holela, sasa ni siasa regulated.
..Je, ni kweli Maraisi wastaafu wa Marekani huwa hawamkosoi Raisi aliyeko madarakani?.
Yes sio hawamkosoi bali hawamkosoi publicly, bali humconsult, lengo la kutomkosoa public ni kuto mu undermine na kumpa uhuru wa kutawala vile anaona inafaa.
Je, Raisi aliyeko madarakani hapaswi kukosolewa na watangulizi wake?.
Nyerere alikosoa publicly kwa sababu alishondwa kuvumilia, it was tuu much. Marais na wastaafu hawapaswi kukosoa public kwa sababu, wanaweza kumu approach na kumshauri, wenye haki ya kumkosoa rais public ni sisi wananchi, rais japo ni kiongozi wetu, ila ni mtumishi wetu, sisi ndio waajiri wake, kupitia kura zetu, na sisi ndio tunaemlipa mshahara kupitia kodi zetu, hivyo tuna haki zote kumkosoa, ila ukosoaji huo ufanyike kwa heshima na lugha ya staha, huku ukishauri, yaani a constructive criticism.

Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
..Je, ni kweli kwamba vyama tawala huwa havikosolewi, isipokuwa wakati wa uchaguzi? kwamba huachwa "viboronge" au vipatie na huja kuulizwa wakati wa uchaguzi tu?.
Siasa ni ushindanishaji wa sera, chama kinashinda uchaguzi kutokana na kukubalika kwa ilani yake ya uchaguzi, hivyo wapinzani wako huru kukosoa utekelezaji wa ilani ya CCM, mwaka mzima na kipindi chote hadi uchaguzi unaofuatia ili kuonyesha maeneo ambayo CCM has failed, ili next time, CCM wasichaguliwe tena, na wachaguliwe wao. Ila katika kupinga sio kupinga tuu kila kitu, bali kwenye maslahi ya taifa, tunu za taifa na dira za taifa, vyama vyote vinapaswa kuwa kitu kimoja.
Na katika kupinga, sio kupinga tuu ili mradi kupinga, bali pinga huku ukionyesha utofauti, ungekuwa wewe ungefanya nini tofauti. Na katika kupinga sio lazima kila siku kupinga tuu, kwenye mazuri, tupongeze
Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri Tupongeze, Rais Magufuli is Changing For The Better!.
..Je, ni kweli kwamba hapa Tanzania kilichokuwa kinaendelea ni MATUSI na siyo siasa za ushindani zinazoshabihisha hoja za wananchi?.
Hajasema ni matusi tuu, amempongeza Lowassa kuwa hajamsikia akitukana. Hata tafsiri ya matusi ni relative, mfano neno mjinga, mpumbavu ni matukano tuu na sio matusi, na kuna matukano mengine ni kweli kabisa, kama mtu ni mjinga na akaambiwa wewe ni mjinga, hapo hujamtukana bali umemwambia ukweli. Ila upinzani wa Tanzania nao, una mambo yake, unakosoa tuu bila kuweka mlinganisho na mbadala.
Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja - Jicho letu, Star TV
..Kama kulikuwa na MATUSI, je suluhisho lilikuwa ni kufungia mikutano ya hadhara?
Kwenye hili la kufungia mikutano, kwangu bado lina ukakasi, kama katiba imeruhusu mikutano, haiwezekani aibuke mtu azuie jambo ambalo limeruhusiwa na katiba.
Na hapa lazima tukubaliane, wapinzani wa Tanzania nao ni wapinzani wa ajabu, kama katiba imeruhusu, halafu mtu amezuia jambo liliruhusiwa na katiba, kwa nini hawajachukua hatua zozote kwa mujibu wa katiba na sheria?!.
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.
My Take.
Kiukweli kabisa, ukiondoa hoja ya kutokukosolewa, haya ndio maneno makubwa kabisa ya busara kubwa kabisa kutoka kwa rais, Magufuli.

Kiukweli kabisa, this man is changing for the better, na akiendelea hivi na busara alioonyesha hapa, inawezekana kabisa, atamaliza akiwa the best president this nation has ever had since Mwalimu Nyerere, kwa sababu maneno aliyoyasema hapa, ni kweli kabisa, yametoka moyoni!. Kuna mengine huwa anayasema kutokea mdomoni tuu!.

Naomba msiniulize nimejuaje yametoka moyoni, na ya mdomoni ni yapi!.
P
 
Last edited:
..JE, huko Marekani uchaguzi mkuu ukiisha mikutano ya kisiasa nayo hufungwa mpaka uchaguzi mwingine?

Hapana. Uchaguzi ukiisha pilika pilika za uchaguzi ujao ndo zinaanza. Mzunguko wao wa uchaguzi hauna kikomo.

..JE, Raisi aliyeko madarakani[ amemtaja Donald Trump] huwa hakosolewi mpaka wakati wa kampeni za uchaguzi?

Anakosolewa sana tu.

Ni hivi, Magufuli siyo stickler wa preciseness. Mara nyingi huwa anaropoka tu bila kujali usahihi wa matamshi yake.

Na siafikiani naye kuwa wabunge wafanye siasa kwenye majimbo yao tu.

Hakuna sheria inayotamka hivyo na kama ingekuwepo ingekuwa ni sheria dhalimu.

Mtanzania yoyote ana haki ya kufanya kazi yake popote pale ndani ya mipaka ya Tanzania.
 
Kiukweli kabisa, ukiondoa hoja ya kutokukosolewa, haya ndio maneno makubwa kabisa ya busara kubwa kabisa kutoka kwa rais, Magufuli.

Kiukweli kabisa, this man is changing for the better, na akiendelea hivi na busara alioonyesha hapa, inawezekana kabisa, atamaliza akiwa the best president this nation has ever had since Mwalimu Nyerere, kwa sababu maneno aliyoyasema hapa, ni kweli kabisa, yametoka moyoni!. Kuna mengine huwa anayasema kutokea mdomoni tuu!.

Naomba msiniulize nimejuaje yametoka moyoni, na ya mdomoni ni yapi!.
P
Napenda ujasiri wako, ila kuwa makini sana,maana unatia vitumbua vya watu mchanga.
 
Huyu jamaa ni mnafiki kuliko kawaida! Anasema Lowassa ni msitaarabu na hatukani, lakini ni yeye huyo huyo alimzuia kabisa hata kufanya mkutano wa kuwashukuru wafuasi wake!
Halafu anadanganya akiwa na macho makavu kabisa kuwa Obama hamkosoi Trump! Hii awamu ni ya uongo hadi hata shetani mwenyewe na uongo wake anasubiri....
 
Back
Top Bottom