Huu ndio uzuri wa mheshimiwa Pombe Magufuli

Shilingi ina pande zote nazo ni muhimu tu sana. Ule upande wa pili unamharibia mema mengi anayoiwazia nchi hii
 
staki kuamini kuwa uwezo wako Wa kufikiri umeishia hapo, na kama kweli uwezo wako umeishia hapo basi Tanzania ya majanga badala ya viwanda inakuja.

by the way, naona kuna nafasi ya ukurugenzi unaisotea maama soon mkurugenzi mmoja atatenguliwa kaza mwendo unaweza kuupata, anzisha Uzi mwingine.

usisahau kumtaja lowasa hili Uzi upate wachangiaji wengi
Tatizo unafuata mkumbo ktk kutathmini mambo, jaribu kuiga mashari
 
kwa mujibu wa kamusi ya oxford komesha maana yake "zuia jambo lisifanyike" na zuia ina maana "fanya isiendelee au isimame" kwa maana rahisi ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma, wanyama kutoroshwa ni vitu ambavyo kwa sasa havifanyiki na vimesimama. kwangu mimi bado kuna walakini sana. kwenye kuboresha nidhamu serikalini na sekta ya elimu hata sijui umetumia vigezo gani! hoja yako ni kichekesho to put it politely. kwenye uso inawezekana ikaonekana vitu viko vizur lakini nyuma ya pazia ni taswira nyingine kabisa.

hivi nidhamu serikalini inakuja kwa kuteua wapiga kelele kwenye nafasi ya utendaji ambazo zina masharti?!

kwa kumalizia ujenzi wa miundo mbinu ya karne ya 21 kwenye miji mikubwa ni bora zaidi kuliko kuhangaika na ununuzi wa ndege ambazo haziwagusi kwa kiasi kikubwa maisha ya mwanachi wa kawaida. hivi ndege moja ya abiria 72 ikianguka hasara yake ni sawa na kipande cha barabara yenye lanes sita kikimeguka?! watanzania huwa hawataki ujinga na usifikiri hawajui yapi ni mapenzi ya kweli kwa mwananchi wa kawaida na matumizi bora ya rasilimali fedha ambayo kila kukicha imekuwa ikiadimika.

lakini sio mbaya kuwa na mapenzi kwa mtu fulani. adios
 
Wanajamvi Leo nimejipa muda wa kutosha kutafakari uongozi wa rais wetu wa awamu ya tano nikagundua kuwa kuna mazuri mengi amefanya kuliko hata mabaya.

Wanasema mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni.

Haya ndiyo mazuri yake:

Amerudisha nidhamu kazini,

Amekomesha uporaji wa fedha za umma,

Ameondoa lundo la michango mashuleni,

Ameboresha elimu,

Ameleta heshima mtaani na nyumbani pia,

Ameongeza ukusanyaji kodi,

Amekomesha ufisadi,

Ameondoa ukilitimba kwenye ajira,

Amefufua shirika la ndege,

Amezuia wizi na utoroshaji wanyama kwenye mbuga zetu.

Amefuta service charge kwenye huduma za umeme.

Na wewe jazia mazuri alioyafanya.

Kumbuka hapa tunazungumzia mema tu.

Nawasilisha.
Joshua Nassari mbunge wa Arumeru hajataka kuwa mnafiki, kaongea ukweli juu ya serikali ya awamu ya tano.

Hivi sasa wanaompinga JPM wanafanana na mrembo anayetongozwa na moyoni tayari keshakubali lakini anaona aibu kuwa muwazi, matokeo yake anajing'ata kidole na kuchuma ua lililo mbele ya macho yake.
 
Lazima uwe na moyo mgumu kama wa Mwendawazimu kumsifia magufuri
 
Siyo kwa enzi za magufuli...eti umsifie akupe Udas au U-dc ..!hakuna zali la mentali kama wewe labda enzi zilee...Juma Poor Manager kavurugwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom