Huu ndio utajiri mkubwa kuliko wote duniani...

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,887
Reaction score
40,069
Kila mtu kwa nafasi yake anausaka utajiri kwa nguvu zake zote na kwa akili yake.Kkila mtu akilini mwake anaamini fedha na mali ndio kila kitu katika maisha yake.Wengi wanaamini kuwa huzuni walizo nazo, mateso waliyo nayo , na mahangaiko waliyo nayo duniani hapa duniani yataondoshwa na fedha.

Kila mmoja hutumia kila mbinu haijalishi ziwe za halali au ziwe za haramu kujipatia fedha na kujilimbikizia fedha.

Kuna watu wameshaitoa sadaka miili yao kwa ajili ya fedha au utajiri.

Wengine mpaka huwa wanawatoa kafara ndugu zao au hata wazazi wao kwa ajili ya mali na fedha.

Lakini cha kushangaza hao wote wanaotafuta fedha na mali wanajikuta bado hawana furaha maishani mwao hata baada ya kupata hizo fedha na mali.

Bado hawana amani ndani ya nafsi zao.

Walikuwa hawajui kuwa utajiri wa mtu na umasikini wa mtu unaanzia moyoni mwake.

Hapa namaanisha kuwa siri ya kwanza ya utajiri ni ridhiko la nafsi yako.

unatakiwa ujifunze kuridhika na kile ambacho unakipata hata kama ni kidogo kwani kwa kawaida mwanadamu hajawahi kuridhika na hatawahi kuridhika mpaka mwisho wa dunia.

Unatakiwa uijaze nafsi yako utajiri ili upate furaha ya kweli maishani mwako.

Kwa kukosa ridhiko la nafsi na roho watu wengi hutumia kipindi chote cha maisha yao kuhangaikia mali ambapo hawapati hata muda wa kufurahia kile kidogo walichovuna kwani kwenye maisha yao wanaamini bado hakiwatoshi.

Si ajabu kusikia mtu ana miezi sita hajakutana na familia yake kwa sababu yupo mbali akizisaka fedha na mali.

Watu wa aina hiyo wao huwa wanaamini kuwa bado wana kipindi kirefu cha kuishi hapa duniani kwa hiyo wanatakiwa wawe na mali nyingi ili waweze kuishi miaka mingi ya amani na furaha hapa duniani.

Siri ya pili ni kumjua MUNGU na sababu ya uwepo wako hapa duniani.

Unatakiwa ujue kuwa hapa duniani mwanadamu ni kama msafiri aliyepumzika chini ya kivuli cha mtu..nikiwa na maana bado safari yake inaendelea na ni lazima iendelee kwani hapa duniani sio makazi yake ya milele bali ni mpitaji tu.

Ndio maana watu kwa kunogewa na ulimwengu hushikwa na bumbuwazi wakisikia mtu amejenga nyumba yake nzuri lakini mtu huyo anafariki siku moja kabla ya kuhamia kwenye nyumba yake.

Ni vyema kila mtu kwa imani yake autafute utajiri wa mbinguni ambapo unaupata si kwa fedha bali kwa kutenda yale yanayompendeza muumba na sio utajiri wa hapa duniani kwani hivi vyote tutaviacha hapa hapa.

Nawasilisha
 
Aisee kikulacho hmenena ukweli mtupu Mimi huwa nawaambia baadhi ya watu Kuwa hebu Kama unajua hapa duniani unapita na mwisho wa maisha yetu ni kuhukumiwa,je una hazina gani mbinguni?ni Kama Kuwa na Alina Fulani ktk bank ya mbinguni,kwa Kufanya matendo mema!mimi huwa napata Amani sana sana Kama nikifanya matendo Fulani ya huruma hata nikiwa sina utajiri na ninachokipata ndo saizi yangu kwa wakati huo!ninaweka asset mbinguni lakini silalamiki,siudhuniki Wala kukosa Amani eti sina gari au nyumba nzuri!mi naombaga sana Afya Njema kwanza!
 
mkuu mleta uzi, hembu sema, ni nini kimekukuta hadi umepata uwezo wa kuleta uzi mzuri hivi, lazima pana kitu.

Ni kitu kinachofanana na hili fundisho kimenipata jioni hii, nilikuwa na jumapili nzur sana. lakini ikaharibiwa. kwa sasa nipo ndani kwangu nahisi kama kumeingia shetani linapitapita ndani.

Ni leo tu mtu mmj alikuja kwa mke wangu mdogo, huyo bwana kamleta mfanyakazi mwenzangu, kiukweli sikutaka mtu hata mmj wa ofisini ajue kwa wake zangu.

Mby zaidi mwanamke mwenyewe alieambatana na bwana huyo ni mbea sana. Nahisi kama alievuliwa nguo.

kwa sasa najibu maswali ya mke mdogo huyu aliyohisi kwa kuyapat kupitia ugeni huu wa leo.

yaan imeniuma sana.
 
Ni kweli hatuna budi kukumbushana mambo kama haya ambayo ni ya msingi zaidi....
 
mkuu mleta uzi, hembu sema, ni nini kimekukuta hadi umepata uwezo wa kuleta uzi mzuri hivi, lazima pana kitu.

Ni kitu kinachofanana na hili fundisho kimenipata jioni hii, nilikuwa na jumapili nzur sana. lakini ikaharibiwa. kwa sasa nipo ndani kwangu nahisi kama kumeingia shetani linapitapita ndani.

Ni leo tu mtu mmj alikuja kwa mke wangu mdogo, huyo bwana kamleta mfanyakazi mwenzangu, kiukweli sikutaka mtu hata mmj wa ofisini ajue kwa wake zangu.

Mby zaidi mwanamke mwenyewe alieambatana na bwana huyo ni mbea sana. Nahisi kama alievuliwa nguo.

kwa sasa najibu maswali ya mke mdogo huyu aliyohisi kwa kuyapat kupitia ugeni huu wa leo.

yaan imeniuma sana.

Hakuna kilichonikuta zaidi ya kuwakumbusha ndugu zangu wapendwa...ili wakae katika njia iliyonyooka .....
 
You just need three things for yo to be happy. Money, health and love. Absence of one is discord.
 
safi mkuu mara moja moja kukutana na somo kama hili linasaidia sana sio kila siku kujadili mstakabali wa nchi akati nchii ndo ipo ivo ivo haijielewi wala nini ndo tukipata madini kama haya ni raha sana..
 
Uliyosema yote no kweli..
But ulipoaanza kuusisha na mambo ya sijui ufalme wa mungu aaaahhhh apo ndio ulipokoseaaa...

Mungu kama kweli yupo Basi ameiacha dunia ijiendeshe yenyewe na mahangaiko yake...

Kwanini watu wanaumwa na kuteseka na maumivu?

Kwanini wengine wanakula wanasaza lakini mtoto mchanga asiye na hatia anateseka na maumivu ya njaa mpaka anakufa?

Kwanini tumeletwa duniani kwenye mateso na kama vile tupo kwenye interview ya mungu kutupima eti kama tunamfata kwa promise ya kuishi huko paradiso firdausi ?

Kwanini mungu asingeweka kitu natural kumuabudu kwa binadamu wote kama ilivo kusikia hamu ya kula vile?

Kwanini inaonekana watu Wa jamii flani ndio Wa mungu hama wao ndio waliooneshwa uwepo wake katika hii dunia...is god a racist?

Kama kweli mungu yupo alikuwa hana haja ya yote hayoo.....
Duniani hapa ure destiny is ure destiny....no matter wat.
 
Ukweli ni kwamba mambo ya Mungu wa kweli ndio chanzo cha baraka zote na maisha yote ya mtu yana maana tu iwapo atamtambua Mungu wa kweli na kuishi maisha sawa sawa na maagizo yake. Nje ya hapo utajiuliza maswali ya kila aina katika dunia hii ikiwa ni pamoja na hayo uliyouliza na kibaya zaidi hutapata majibu yake.
 
Tumia kipawa ulichojaaliwa kusaidia watu.Tumia kipawa ulichojaaliwa kutenda mema.Tumia kipawa ulichojaaliwa kumfurahisha MUNGU.Tumia kipawa ulichojaaliwa kuingia Peponi.
 
Ukweli ni kwamba mambo ya Mungu wa kweli ndio chanzo cha baraka zote na maisha yote ya mtu yana maana tu iwapo atamtambua Mungu wa kweli na kuishi maisha sawa sawa na maagizo yake. Nje ya hapo utajiuliza maswali ya kila aina katika dunia hii ikiwa ni pamoja na hayo uliyouliza na kibaya zaidi hutapata majibu yake.

So you're talking abt Baraka zote na maisha yote ya mtu.....

So ukimtambua mungu Wa kweli hautaishi kwa tabu?
Au unamaana gani

Try kujibu maswali japo mawilii?

Nmesoma Dini zote mbili bado sijapata majibu ya hayo maswali...uislam na ukristo.
 
Khaa!! Mwisho nikajua utasema tumtolee bwana (sadaka)
Pepo na moto hapahapa duniani. Afya na furaha hutengenezwa. Kama una source ya income, dem wa kupiga na ujuzi unaotumia kuwasaidia binadamu wengine tayari uko peponi na kinyume chake ni motoni full stop
 
Uliyosema yote no kweli..
But ulipoaanza kuusisha na mambo ya sijui ufalme wa mungu aaaahhhh apo ndio ulipokoseaaa...

Mungu kama kweli yupo Basi ameiacha dunia ijiendeshe yenyewe na mahangaiko yake...

Kwanini watu wanaumwa na kuteseka na maumivu?

Kwanini wengine wanakula wanasaza lakini mtoto mchanga asiye na hatia anateseka na maumivu ya njaa mpaka anakufa?

Kwanini tumeletwa duniani kwenye mateso na kama vile tupo kwenye interview ya mungu kutupima eti kama tunamfata kwa promise ya kuishi huko paradiso firdausi ?

Kwanini mungu asingeweka kitu natural kumuabudu kwa binadamu wote kama ilivo kusikia hamu ya kula vile?

Kwanini inaonekana watu Wa jamii flani ndio Wa mungu hama wao ndio waliooneshwa uwepo wake katika hii dunia...is god a racist?

Kama kweli mungu yupo alikuwa hana haja ya yote hayoo.....
Duniani hapa ure destiny is ure destiny....no matter wat.

Mungu kakuumba mwnadamu akakupa akili ya kujua mema na mabaya.. So tenda mema,usiwaze sana kuhusu wafuasi wa ibilisi maana wamekwisha kuhukumiwa.

Tenda mema,wacha maswali zenye hazina mashiko.
 
Back
Top Bottom