Sikununu,
Kweli umesoma dini zote uislam na ukristo?
Kuna kitu kinaitwa kudra za mwenyeeziMungu za kheri na za shari je unazijua? Na kuziamini?
Na katika moja wapo ya nguzo za dini kuna inayosema tutoe zakka kwa mafakiri na maskini je binaadam tunaitekekeza? je kwenye matatizo tunasaidiana?
Huoni kuwa ni sisi binaadam ndo tuno create matatizo kwa asilimia kubwa duniani? Kwa sababu hatufuati maamrisho ya Mungu, tajiri atataka ajilimbikizie mali zaidi na zaidi na kusahau kama kuna mafakiri wanataka kusaidiwa. Au mtu anamuua mwenzie kwa sababu ya kitu, mwenye kushiba hataki hata kumuangalia mwenye njaa. Watu tuna hasad.
Kwa sasa naomba niishie hapo