Ni vile tu watu hamtaki kujifunza. Toka zamani na zamani kwenye utamaduni wa Mwafrika kulea familia sio jukumu la mwanaume, hilo ni jukumu la mwanamke (mama).
Na ndio maana ni mwiko mwanaume wa Kiafrika aliyeoa kuingia jikoni na kupika, pia hata zamani wanaume walikuwa wanaoa wanawake wachapakazi wanaojua kulima ili tu wakawalimie mashamba yao.
Kiufupi wanaume wao walikuwa na bado wanatafuta wake wakwenda kuwalea.
Jiulize kwanini mwanaume wa kiafrika anaoa mwanamke ambaye kiumri ni mdogo kwqke ni ili tu anavyoendelea kuzeeka na kupoteza nguvu awe na uhakika wakulelewa.
Ni kweli familia nyingi za kiafrika wanawake ndio walezi wakuu na hata mtoto akiwa na tabia mbaya shida ni mama, baba akiwa anaugua au ana afya dhaifu shida ni mama, ila mwanamke akiwa na afya dhaifu au akiwa anaugua shida ni yeye au wake wenza wamemloga.