Huu ndio ukweli ambao walinda legacy hawataki kuusikia!

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,730
11,079
Mara utasikia Hayati ameacha miradi mingi. Hiyo miradi ni ipi? Kila Rais aliyetawala nchi ya Tanzania kuna jambo muhimu alilofanya, hakuna Rais alieitawala nchii hii akamaliza muda wa uongozi bila kufanya lolote kulingana na sera ya chama.

Mambo ambayo walinda legacy ya Hayati hawataki kuyasikia kabisaa kumhusu Hayati na miradi yake;

(1) Fedha zilizotumika kwenye miradi hasa ujenzi wa madaraja mfano Daraja la Busisi, baadhi aliwadhurumu matajiri, matajiri na wafanyabiashara wakubwa walilala matajiri na kuamka masikini.

Pesa kwenye account zao za benki zilikombwa tu na hata walipojitahidi kuzipigania walitishiwa kupewa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha.

(2) Matajiri wengi na wafanyabiashara walifirisiwa kwa kigezo kuwa ni wakwepa kodi wakubwa jambo ambalo halikuwa na ukweli hata kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom