Huu nao ni aina ya utapeli, unamuazima mtu pesa akiwa mstaarabu ila kurudisha anakuwa mkaidi

Kutolipwa kunauma pale ambapo uliemkopesha ana kauli mbaya, unamdai mtu anakwambia we nawe hicho ki ef50 kelele zote hizi,au unapokea matusi
-Ustaarabu kitu chema sana,
- uungwana ni vitendo
-Maneno mazuri yalimtoa nyoka pangoni
Hivi ukipokea simu ukamweleza kistaarabu anaekudai kwa yanayokusibu pengine ukashindwa kulipa unapungukiwa nini? kuna watu wastaarabu kiasi kwamba kama mnafanya biashara ukimfata akupe hela yako anakwambia kistaarabu kiasi unakuta labda ana watoto hawajala tangu jana unachukua tena hela ingine unawanunulia maandazi wanywe chai.

watu wenye kauli mbovu wanatukosesha sana mkopo sisi ambao hatuna mishahara ya kuweka rehani
 
WanaJF kwenye maisha Kuna viatu na watu.

Najuta hivi inakuwaje mtu anapokuwa na shida anakuja kwako umsaidie kiasi cha fedha na akasema atakurudishia lakini wakati unampa unamuona mtu mstaarabu Sana.

Leo kwenye kurudisha ni shida yaani nikipiga simu kwa kutumia simu yangu hapokei, nikitumia namba ngeni anapokea huu si aina ya utapeli mpya?

Nimejifunza kitu kwenye pesa ukiamua kumsaidia mtu Bora umpe tu kuliko kumuazima maana ukimwazima pesa mwishoni utakuja kugombana leo hii ndiyo nimeamini!
Ni vzr kumpa tu kama kufanya sadaka kukopeshana ni lawama sana mkuu..mfano mie mtu akisema nikope lk 1 namwambia ntakupa elf 50 sitokudai ndio utaratibu wangu spendi stress za kudaiana kbs mnaweza potezana hadi udugu au urafiki!
 
Ndiomaana ukilipa deni unaandikiwa thawabu,Inahitaji uwe na moyo wa kipekee kulipa pesa uliyokwisha itumia.

Aghalabu utaona kama sihaki kuilipa, hapo ndipo udugu na urafiki utaanza kutetereka.

Nna jamaa zangu kadhaa nishawaazima hizi hizi 40,50 lakini tunakutana miezi inakatika hata habari hawana.

Kuna ndugu zangu mmoja kwenye 200,000 akarudisha 50,000 nyingine miaka inaondoka sasa, mmoja 20 ikamkimbiza kabisa .

kiukweli imeshatengeneza kitu kwenye nafsi yangu. Japo moyo wa huruma na kujali kuuondoa hua ni ngumu ukiwa nacho nafsi hua inakusuta sana kumnyima mwenye uhitaji.
 
WanaJF kwenye maisha Kuna viatu na watu.

Najuta hivi inakuwaje mtu anapokuwa na shida anakuja kwako umsaidie kiasi cha fedha na akasema atakurudishia lakini wakati unampa unamuona mtu mstaarabu Sana.

Leo kwenye kurudisha ni shida yaani nikipiga simu kwa kutumia simu yangu hapokei, nikitumia namba ngeni anapokea huu si aina ya utapeli mpya?

Nimejifunza kitu kwenye pesa ukiamua kumsaidia mtu Bora umpe tu kuliko kumuazima maana ukimwazima pesa mwishoni utakuja kugombana leo hii ndiyo nimeamini!
Kwl kbx
 
Sitarudia kukopesha kitu kinaitwa mwanadamu, hela zangu zinaniuma sana nilizodhulumiwa
Binafs sitokopesha Tena hela zangu nying nimepoteza kupitia kujifa ya kusaidia wenzangu nimeshindwa hata Kula vizur ili niwasaidie wenzangu!
 
Back
Top Bottom