Huu mwaka 2023 ni kama umekwisha, umefanya nini cha maana?

Kiukweli kitu pekee cha maana nilichokifanya ni kurudiana na mwanaume wa maisha yangu.

Baada ya kugundua nilipotea nilijirudi, nikaomba msamaha na hivi sasa maisha yamekuwa na maana kila kitu kinaenda sawia kwa mapenzi & amani anayonipa. Sijui nilifeli wapi haki!

Ila nimejifunza, sitorudia tena. Mwaka 2023 umekuwa bora sana kwangu, Mungu ni mwema.
Umefanya vizuri sana, wanaume tunapenda sana wanawake watiifu, wenye kuleta amani ndani ya nyumba na wanaojishusha

Sura nzuri na tako bila heshima ni ngumu kudumu kwenye ndoa

Somo zuri kwa wanawake wengine, kila la kheri unapoanza mwaka 2024
 
Ni mafanikio pia hongera mkuu... kwasababu Kuna ambao hata hawajaweza kulipa hiyo karo unayosema
mm nadhani maendeleo ni kufanya jambo jipya. Kwa mfano ujenzi mpya au mwendelezo, kununua mfuga kwa sisi wenye makazi vijijini, kununua shamba, kuongeza kiwango cha akiba ya fedha, kufungua biashara mpya au kukuza mtaji wa biashara nk.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli kitu pekee cha maana nilichokifanya ni kurudiana na mwanaume wa maisha yangu.

Baada ya kugundua nilipotea nilijirudi, nikaomba msamaha na hivi sasa maisha yamekuwa na maana kila kitu kinaenda sawia kwa mapenzi & amani anayonipa. Sijui nilifeli wapi haki!

Ila nimejifunza, sitorudia tena. Mwaka 2023 umekuwa bora sana kwangu, Mungu ni mwema.
Hongera
 
Asante sana.
Katika watu wote wewe ndio umenihoji maswali ya msingi, bless up.
Shukrani sana!

Mahusiano ya sasa yana changamoto nyingi sana lakini changamoto kubwa zaidi ni kutokukubali 'kujishusha' kwa wale wanaohusiana.

Nimeshuhudia mahusiano mengi mazuri yakifa na sababu kubwa ni pande mbili kutaka kuoneshana ubabe na ubora. Ukiwakalisha chini usuluhishe kila mmoja analeta mlolongo wa makosa ya mwingine na kila mmoja anaamini makosa ya mwenzake ni mazito na hayavumiliki, ni afadhali makosa yake.

Katika kuhusiana, ni vizuri sana kujishusha na kuombana msamaha kuliko kuonyeshana 'ukijike' na 'ukidume' na kuondoa kiburi cha kuonyeshana "nina options, sio wewe tu unayeniona"
 
Back
Top Bottom