Huu mwaka 2023 nakubali nimekwama

Mfilisiti

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
342
1,551
Wakuu natumai kila mtu Mungu wake anampigania kwa imani yake, niende kwenye mada.
Huu mwaka pindi unaanza niliweka malengo, lakini ukweli nikuwa "unaweza ukafanya kila kitu kwa usahihi na bado ukafeli vile vile"
Mwaka unaisha na mambo yamekwama, sometimes natamani ningekua kuna hela naisikilizia labda ingenitia moyo ila wapiii😂😂

Nilichukua heka tano huko Namtumbo kwa ajili ya kilimo cha mahindi ila sasa kwa hali ilivyo hata heka moja tu kuilima ni mzozo

Pengine 2024 itakua na neema kwetu, Wanangu wasongokaji Mungu hajamalizana nasi.

Account imenuna 😏😏kabisaaa
PXL_20231204_164829193~2.jpg
 
Nilifanikiwa kufungua ofisi niliyokua naitamani kipindi chote cha maisha yangu. Ila ilikufa kiajabu sana mpaka sasa sina hamu😔
Ni jambo la kawaida kabisa kuanguka mara nyingi kabla hujafikia mafanikio.

Kila mtu ana majira yake.

Yakifika majira yako pesa itakutafuta yenyewe na hutaamini
 
vijanaaaaaaaa😁😁😁😁😁😁ooh namtaja nikifikisha miaka 25 tuu niwenanyumba Kali gari nafamilia Bora Kiko wapi?unamiaka mingapi broo 30 au?
Kufanikiwa na umri havina uhusiano wowote, bado sijafika 30
 
Wakuu natumai kila mtu Mungu wake anampigania kwa imani yake, niende kwenye mada.
Huu mwaka pindi unaanza niliweka malengo, lakini ukweli nikuwa "unaweza ukafanya kila kitu kwa usahihi na bado ukafeli vile vile"
Mwaka unaisha na mambo yamekwama, sometimes natamani ningekua kuna hela naisikilizia labda ingenitia moyo ila wapiii😂😂

Nilichukua heka tano huko Namtumbo kwa ajili ya kilimo cha mahindi ila sasa kwa hali ilivyo hata heka moja tu kuilima ni mzozo

Pengine 2024 itakua na neema kwetu, Wanangu wasongokaji Mungu hajamalizana nasi.

Account imenuna 😏😏kabisaaa
View attachment 2842399
Wala usijali hio haina kukata tamaa maadam afya iko njema basi kuna TUMAINI bado. Mungu akutangulie
 
Back
Top Bottom