GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,443
- 120,800
Nimeshangaa sana hadi sasa hivi najiuliza na sipati majibu kwani muda si mrefu matokeo yetu ya Mtihani wa Kozi moja hivi ninayoifanya yametoka online na kuna njemba fulani zinaijua namba yangu ya Mtihani wamenipigia Simu huku wakiwa wanacheka huku wakiniambia kuwa Mimi na Wao tume Bashite hivyo eti tunatakiwa kufanya Kimeo chetu cha Sup siku ya Jumanne.
Kama hiyo haitoshi juzi Ijumaa wakati napita pembezoni mwa Shule moja ya Sekondari nikamsikia kwa masikio yangu Mwalimu Mkuu wao akisema naomba nimnukuu " Nyie Wanangu Shule nzima tunawaamini hivyo mwaka huu katika Mtihani wenu wa kumaliza Kidato cha nne hatutaki mtuletee Mabashite mengi hapa kwani mtakuwa mmetuaibisha sana na sijui tutaficha wapi hizi sura zetu " mwisho wa kumnukuu.
Naomba nipatiwe maana na dhana nzima ya huu Msamiati mpya na ambao naona unaanza kushika kasi wa neno Bashite kwani binafsi mpaka sasa sijajua una maana gani ila nikaona kwakuwa humu JF kuna Great Thinkers wa kutukuka kabisa basi sitakosa majibu yake.
Nitawashukuruni na nawasilisha.