Tujadili suala hili katika picha mbili, Afrika (kama bara) na Tanzania (kama nchi mwanachama). Kwa sasa rais wetu JK ana kofia mbili, moja ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (yaani AU), na pili ndiye rais wa Tanzania yetu (mwanachama wa AU).
Inapotokea kuna matatizo (kama vita, machafuko, ghasia na matatizo mengineyo) katika nchi mwanachama wa AU, AU kama taasisi hufanya tathmini ya kujua nini kifanyike ili kuondokana na matatizo hayo!
Kama ni machafuko ya kisiasa (ubabe wa kiongozi mmojawapo) kama yaliyotokea kule Comoro, AU inachokifanya ni kutuma askari wa kutuliza ghasia na kumuondoa madarakani huyo kiongozi. Ili kufanikisha hilo, inahitaji askari (either wa miguu, angani, au majini), inahitaji magari ya kivita, vifaru, na wakati mwingine hata ndege ya kivita! Pia, inahitaji silaha za aina mbali mbali (kama vile, risasi, mabomu na kadhalika).
Hapa naomba ieleweke kitu kimoja, taasisi hii (AU) haina ndege ya vita, Jiefang, wala kifaru!! Yenyewe ina wataalamu tu wa kufanya tathmini (wengi hawalifahamu hili)!!
Mara baada ya kufanya tathmini na kutuma ripoti kwa watendaji wa juu (Mwenyekiti akiwa mmojawapo, kwa sasa JK), uomba nchi wanachama (wa AU) mwenye uwezo wa ku-provide hayo mahitaji!
Ndipo hapo nchi kama Tanzania hujitokeza na kusema, nita-provide
askari wa miguu - 47
askari wa majini - 12
vifaru - 2 na kadhalika! Na nchi nyingine pia itajitokeza, mpaka hapo yale mahitaji yote yaliyopendekezwa kwenye tathmini yatakapokamilika! Kisha msafara unaanza ...
Kama mnavyoelewa sasa AU (kama taasisi) haina askari wala kifaa chochote cha kivita, kwa hiyo inachokifanya kwa nchi zilizojitolea hivyi vifaa pamoja na askari wake, ni kuwalipa pesa kwa gharama ya kila kifaa (kwa thamani ya sasa ya dukani, i mean brand new!). Kama Tanzania walipeleka Kifaru (kikuu kuu cha mwaka 2001), basi hujakulipwa Kifaru kipya kwa thamani ya bei ya Kifaru kwa leo (2008). Na hii ndio "bonus pekee" inayofanya majeshi mengi ya nchi za Western & Central Africa kuchangamkia inapotokea shughuli kama hii!
Suala la pili ni askari, hawa huwa na mkataba maalunm kwa ajili ya kazi hii, ambao huwa nje ya mkataba wake wa sasa wa kazi na JWTZ! Ambapo sijahamu figure kamili lakini husemekana ni mnono sana!
Sasa tukirudi kwenye mada, Tanzania (kama mwanachama wa AU), kutokana na majeshi yale kufanikiwa, basi inajivunia nchi mwanachama mwenzetu kupata utulivu, na tunasikia sasa wanapanga tarehe ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasi (sote tunaamini hili ni jambo zuri). Kwa upande wa JK, yeye kama Mwenyekiti wa AU, may be alikuwa na maono (for the 1st time) kwamba hapa jeshi ni muhimu kuliko mazungumzo yasiyokwisha yaloyokuwa yakisimamiwa na Thabo Mbeki! Na hapa nakuthibitishia JK amezoa heshima nyingi sana dhidi ya Mbeki (alipinga hapo mwanzo kuhusu matumizi ya jeshi ktk suala hili)!
Pili Tanzania kama nchi, nilishapata kuzungumza na "mkuu" mmoja wa jeshi kuhusu suala la kutoa majeshi yetu kwenda kulinda amani, akanieleza masikitiko yake kuwa Tanzania tumezubaa sana tunashindwa kuchangamkia "tenda" hizi, kwani zina manufaa sana kwa upande wa vifaa vya kijeshi (kama nilivyozungumzia "bonus")!! Pili alinieleza askari wa kwenda huko sio shida, kwani wao wenyewe ndio hujitokeza kwa wengi kuomba kwenda (kutokana na "marupurupu" ya shughuli hiyo)! Sasa baada ya shughuli hii, JWTZ inakwenda kupata malipo yake ya vifaa vyote ilivyopeleka Comoro (whether zimeharibia na kuachwa huko comoro au vimerudi na vinaendelea kutumia makambini kwao JWTZ!). Italipwa kwa vifaa vyote!
Kuhusu askari kufa kazini, jamani hakuna kazi isiyo na "ajali kazini"! Na hakuna anayependa hilo litokee, iwe kwenye kazi yeyote! Kwa sasa, sote kama wananchi wa TZ tunatakiwa tutambue mchango waJWTZ na kutoa rambi rambi wa huyo askari mmoja aliyepoteza maisha.
Naomba kuwakilisha.