Hussein Bashe aongea na vyombo vya habari

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Atatoa ufafanuzi wa mambo kadhaa kama itakavyoonekana kwenye 1st post kwenye hii topic. Nitawa-update juu ya kinachoendelea kwenye kikao hicho.

bashe.jpg


============

UPDATES:

  • Kikao ndo kinaanza.

  • Anasema kamati ya UVCCM iliyoundwa ku-reform si kamati ya kujivua gamba. Anajaribu kutoa ufafanuzi.

  • Tumeamua kufanya reform kipindi hiki ambacho bado UVCCM ina ushawishi ndani ya jamii na bado CCM ipo madarakani nchi bado ina amani na utulivu.

  • Anatoa ufafanuzi juu ya kwanini kamati ya reform iliundwa ndani ya UVCCM na anatoa historia ya wapi wametoka na kwanini wamefikia hapa.

  • Anasema UVCCM itashirikiana na vijana wa kada zote kuanzia wamachinga mpaka vijana wasomi. Wawe wa CCM au wasiwe wa CCM provided CCM ndicho chama tawala! Kwa maelezo ya Bashe, watatumia asasi za kiraia zinazojihusisha na siasa kuijenga/iimarisha UVCCM. Kamati yake itatoa taarifa ya kazi yake mwezi Julai kama ilivyotakiwa kufanya. Anajaribu kutoa ufafanuzi juu ya namna watakavyofanya data collection. Anasema FaceBook na mitandao ya kijamii vitatumika pamoja na Public hearing katika kufanikisha azma.

  • Anaulizwa juu ya mafisadi watatu Rostam, Chenge na Lowassa, wao kama UVCCM wanasemaje juu ya magamba haya!

  • Anasema suala la 'magamba' limetolewa ufafanuzi na Katibu mkuu wa CCM na hivyo hadhani kama kuna suala la mtu kufukuzwa mtu ndani ya CCM. Anasema yeye si msemaji mkuu wa CCM (NEC) lakini anaamini Mukama anaweza kulitolea ufafanuzi hilo.

  • Kaulizwa kuwa suala la kufukuzwa mafisadi lilianzia UVCCM na sasa CCM ikawa inaelekea kwenye utekelezaji, anaongeleaje juu ya hili?

  • I got disconnected, natumaini maswali yote aliyoulizwa pamoja na la uraia wake yatajibiwa!

  • Suala la uraia amelitolea ufafanuzi, kuwa wagombea wakati wanaenda kwenye kura za maoni wangechujwa kabla ya kupelekwa kwa raia ili masuala yenye mashaka yaepukwe. Ameisifia CCM kwa kuamua kumwondoa kuepuka risk lakini baadae kumsafisha kuwa uraia wake hauna utata kupitia kwa waziri aliyekuwa na dhamana.

  • Kaulizwa kwanini CCM haikumsafisha akasafishwa na serikali; kasema chama hakina mamlaka ya kumsafisha.

  • Suala ya yeye, Shigella na Ridhiwani kudaiwa ni mafisadi kasema ni maoni ya watu. Ila akasisitiza ndani ya CCM pamevamiwa pia na yeyote sasa anaweza kuongea na vyombo vya habari na kutoa taarifa tu!

  • Anasisitiza mkakati wa kuchafuana ndani ya UVCCM unajulikana unasukwa na nani na anaye-finance anajulikana kwani dhamira yake ni urais 2015. Ametuma vijana Iringa, Mbeya, Ruvuma na anaendelea kuwatumia wengi. Itafika wakati watalazimika kumtaja hadharani.

  • Kaulizwa kama wataitumia JF kakiri kuwa wataitumia pia kukusanya maoni ya wananchi kuelekea kuifanya UVCCM irejeshe heshima yake na ku-appeal kwenye public.
 
Naendelea mkuu, bado anawataja waliochaguliwa/teuliwa kuwa kwenye kamati yake ndani ya UVCCM
 
Kama huna habari kamili kwa nini unaanzisha thread mkuu...ungesubiri hadi uwe na hiyo habari..
 
Eti nani, Bashe?? Kwani Bashe ana lipi la maana la kutuambia kwenye vyombo vya habari???
 
Natumaini atatoa ufafanuzi juu ya suala la uraia wake (hajawahi kuongelea hili)
 
hii ndiyo JF. sisi hatuna kusubiri vikao vya chama.

Heshima mbele mkuu, heading ya hii thread haiendani na content yake, Inv kaandika "H. Bashe aongea na vyombo vya habari" wakati jamaa hata kwenye kiti alikuwa hajakaa, angesubiri apate content then aanzishe thread.
 
Kama huna habari kamili kwa nini unaanzisha thread mkuu...ungesubiri hadi uwe na hiyo habari..
....ushaaambiwa hii ni LIVE thread, tulia upewe vitu kutoka jikoni, same time same place as they happen.
lete News Mkuu usieonekanaga
 
Tumeamua kufanya reform kipindi hiki ambacho bado UVCCM ina ushawishi ndani ya jamii na bado CCM ipo madarakani nchi bado ina amani na utulivu.

nimeipenda sana statement hiyo. anakiri kuwa ushawishi huo untoweka hahaha!

mimi ni mwanajamii. sijawahi kushawishika na taasisi yoyote ya CCM tangu ning'amue kuwa CCM ni genge la nguruwe wanaotafuna shamba letu (rasilimali za nchi yetu).
 
nimeipenda sana statement hiyo. anakiri kuwa ushawishi huo untoweka hahaha!

mimi ni mwanajamii. sijawahi kushawishika na taasisi yoyote ya CCM tangu ning'amue kuwa CCM ni genge la nguruwe wanaotafuna shamba letu (rasilimali za nchi yetu).
Mkuu,

Jamaa wanaonekana wanaamini wana ushawishi mkubwa, kama hujashawishiwa wewe basi huenda kuna mamilioni ya watanzania wamefanikiwa kuwashawishi kama wanavyoainisha hapo juu.

Najaribu kushawishika pia lol
 
Back
Top Bottom