Je, unaijua vita yako ya kiroho?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,514
Habari wakuu,

Kama ulikuwa hujui basi jua sasa ya kuwa unavita ya kiroho.

Vita hii uwe unaiona au auioni ila ipo inaendelea kwenye Ulimwengu wa Roho.

Uwe unajua au hujui vita ya kiroho ni lazima upigane.

Vita ya kiroho ni Nini? Hii ni vita ambayo inapiganwa katika Ulimwengu wa Roho. Vita hii huonekana zaidi katika ndoto au maono.

Vita hii ya kiroho watu huota au huona maono wakiwa wanakimbizwa au kupigwa na watu au wanyama na wakati mwingine hupigwa au hupigwa.

Wapo ambao wanauwezo wa kuona na kushindana na vita hizo ila ni wachache sababu bawa wanakuwa wanaukaribu na na Mungu na Roho Mtakatifu anawasaidia.

Neno la Mungu linasema Efeso 6:11
Vaeni silaha zote muweze kumshinda shetani. Maana kushindana kwetu sisi SI kwa damu na nyama bali ni kwa falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza...

Watu gani ambao unapigana nao ktk Ulimwengu wa Roho ni wakuu wa giza yaani wachawi, mizimu na majini nk.

Watu wengi wamekuwa wakidhani adui ambaye anakuwa anapigana nae ktk ndoto basi ni mtu wa mbali.

Hapa ndio panapofanya mtu azidi kutofahamu kuwa anapigana na nani.

Neno la Mungu linatuambia ya kuwa adui wa mtu ni wa nyumbani mwake.
Mathayo 10:36

Ni hivi ukiona unapata vita ujue hiyo vita haitoki mbali bali ipo ndani ya familia au ukoo wako ndio wanaokujua.

Moja wapo ya njia sahihi ya kumjua adui yako ni kuomba Roho Mtakatifu akuonyeshe, pia kuomba hekima ya Mungu maana kumjua adui si jambo dogo unaweza ukatumia sheria mkononi.

Siku hizi Mungu amewaleta Manabii wake yaani wamepakwa mafuta wenye macho ya Rohoni wanaona.

Wamekuwa wakiona na kuwaambia watu kuwa vita yako imeanzia kwa mf; mama yako mzazi, bibi yako, mtoto au mizimu nk.

Pia Manabii hao wamepewa mamlaka na ya kuwaondoa watu katika vita.

Ikumbukwe pia kuna Manabii wa uongo.

Mnisamehe kama sikuandika ipasavyo ila najua hapa kuna walimu wa neno watakuja kutupa maelekezo zaidi...

Mbarikiwe na YESU alie hai

Mwl Mwakujonga
 
Inahitaji kuuchagua upande wa Amani na kuacha kuongelea upande wa Vita

Hii ndo njia sahihi na mathubuti ya kuishinda Vita ya Kiroho.

.kile unachokipa Nguvu na kukiongelea Sana ukaa katika (Subconscious mind) na hi Inawezekana ukawa Mlokole lakini ukawa unasumbuliwa na huyo Shetani.

Kwakuwa ulimwengu/Dunia ipo katika Duality ,Uwili uwili unabidi kulivaa vazi moja na sio mawili hivyo Kati ya UPENDO na chuki unaweza kuchagua UPENDO na ukichagua upendo hakikisha hautoi UPENDO wa masharti . Pia ukichagua Malaika na Shetani hakikisha haumuongelei Shetani unamuacha Kama alivyo usimpe Nguvu katika kinywa chako so badala ya kumkemea unaweza tumia huo Muda kuomba baraka za MUNGU ziwe kando yako 24/7.
 
Hizo vita ni walokole wanavsababisha kukemea kemea ovyo mwisho wa sku wanatengeneza negative vibe , angalia maisha ya wanaokemea kemea ovyo na kujifanya wana mkanyaga shetani .
 
Inahitaji kuuchagua upande wa Amani na kuacha kuongelea upande wa Vita

Hii ndo njia sahihi na mathubuti ya kuishinda Vita ya Kiroho.

.kile unachokipa Nguvu na kukiongelea Sana ukaa katika (Subconscious mind) na hi Inawezekana ukawa Mlokole lakini ukawa unasumbuliwa na huyo Shetani.

Kwakuwa ulimwengu/Dunia ipo katika Duality ,Uwili uwili unabidi kulivaa vazi moja na sio mawili hivyo Kati ya UPENDO na chuki unaweza kuchagua UPENDO na ukichagua upendo hakikisha hautoi UPENDO wa masharti . Pia ukichagua Malaika na Shetani hakikisha haumuongelei Shetani unamuacha Kama alivyo usimpe Nguvu katika kinywa chako so badala ya kumkemea unaweza tumia huo Muda kuomba baraka za MUNGU ziwe kando yako 24/7.
Umeongea vitu muhimu na principles za maumbile wachache watakuelewa.
 
Mmeanza.Muhimu ni kusali tu Mungu ni mwema na mwaminifu sana,ukimtumainia yeye huwezi kuogopa chochote iwe kinaonekana au hakionekani.
 
Inahitaji kuuchagua upande wa Amani na kuacha kuongelea upande wa Vita

Hii ndo njia sahihi na mathubuti ya kuishinda Vita ya Kiroho.

.kile unachokipa Nguvu na kukiongelea Sana ukaa katika (Subconscious mind) na hi Inawezekana ukawa Mlokole lakini ukawa unasumbuliwa na huyo Shetani.

Kwakuwa ulimwengu/Dunia ipo katika Duality ,Uwili uwili unabidi kulivaa vazi moja na sio mawili hivyo Kati ya UPENDO na chuki unaweza kuchagua UPENDO na ukichagua upendo hakikisha hautoi UPENDO wa masharti . Pia ukichagua Malaika na Shetani hakikisha haumuongelei Shetani unamuacha Kama alivyo usimpe Nguvu katika kinywa chako so badala ya kumkemea unaweza tumia huo Muda kuomba baraka za MUNGU ziwe kando yako 24/7.
Ni kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom