Hunter hunted - Simba agonga mwamba kwa nyati

Hunter hunted - Simba agonga mwamba kwa nyati

Huyo simba alishachoka na maisha yaani hadi nyati jike amemvimbia kiasi hicho mpaka ame "mdedisha"!
 
Siku zote timu ya simba ndio huwa inafanikiwa kumdhibiti nyati mmoja,tofauti na hapo,haiwezekani.

Nyati ndiye mnyama chaguo la mwisho kuliwa na simba,baada ya wengine kutoonekana,maana shughuli ya kumuangusha simba wanaijua.

Na katika hali kama picha inavyoonekana ni kwamba,nyati nayeye anakuwa alikuwa amepania kumuua simba,yaan unakuta simba anjaribu kukimbia lakini jamaa hampi nafasi,sio kwamba simba alikuwa anataka kumshika nyati/hawezi jaribu akiwa peke yake,ni kama ajari anajikuta kizuizini.
 
Huyo nyati atakuwa shabiki wa Yanga...
 
Mbogo huwa hana mchezo simba mmoja hawezi kumuua lazma waje wa4 mpka wa5 ndio wamuweze mbogo
 
Mbona iyo ni kawaida tu..
Simba kibao.wanauawa na nyati.
Video zpo nyng tu Youtube.
Huyo ana bahati kafa vizuri,kuna video moja simba ameingia katikati ya nyati kama 200.
Wakaanza kumrusha juu na kumtifua kisawasawa na mapebe yao mpaka mwisho wa siku simba kawa vipande vipande.

Mpwa naifahamu ile video aiseee, simba alichezea kichapo cha haja, walimrusha juu kama mpira wa kona halafu wanapeana zamu ya kupiga
 
Huyu simba kwa kumtazama tu......ni bado mdogo.......kwa makadirio ana miezi kadhaa kuelekea mwaka........simba huwa ma maumbo makubwa kadiri wanavyokua.........so atakuwa ni dogo katika jitihada za kupanua mbavu.......akachezea balaa nyati tornado ......!
 
Back
Top Bottom