Ukisoma hii habari utaona sababu inayotolewa ya watu kutaka kujiunga CHADEMA ni CCM kushindwa kukamilisha ahadi za mipango ya maendeleo.
Kiundani, hawa watu hawajajiunga CHADEMA zaidi ya kuondoka CCM na kuingia chama kingine kilichoonekana karibu.
CHADEMA inabidi isibweteke na kufurahia tu wanachama wapya, inatakiwa kufanyia kazi sababu zilizowafanya wanachama hawa waondoke CHADEMA.
Mie mwenyewe nimeenda huko vijijini, nimeona watu wana mwamko wa kuingia CHADEMA hata kabla ya kuijua vizuri CHADEMA ikoje.
Huu ni mtaji mkubwa wa kisiasa kwa chama chochote cha kisiasa.
CHADEMA msiufuje na ku disappoint wananchi.