Huna ajira? Pitia hapa, chukua hatua

Huna ajira? Pitia hapa, chukua hatua

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
180
Wanabodi na vijana wenzangu.

Kama huna ajira fanya yafuatayo na uchukue hatua;

1. Tafuta Tsh 200,000 tu.
2. Tafuta eneo la kuchoma viazi/chips hasa karibu na vyuo, msongamano wa watu.
3. Fungua hii biashara ya kuuza chips usione aibu wala kuogopa.
4. Jipe mwaka mmoja tu. Utakuja kuniambia.

Kama hiyo haitoshi, kuna fursa ya kuuza Juice ya Miwa. Nenda SIDO chukua mashine ya kusaga juisi ya miwa tafuta eneo lenye mkusanyiko wa watu nunua grass zako 10 na Ki-meza.

Ukithubutu Tanzania hakuna umaskini, ukiona unaogopa tafuta kijana mpe mtaji msimamie tafuta mkopo wa Tsh 400,000 kwa biashara ya kuuza JUISI YA MIWA. Ni biashara ambayo haina usumbufu wa TIN NO, LESENI YA BIASHARA, WALA KODI YA FREMU.

Mimi binafsi nimeajiri vijana wanachoma viazi/chips na kunipa 20000 kwa siku kama maeneo matano. Mtaji nilianza nao kwa kila kijana 150,000 kodi ya kieneo kwa madalali 1000 kwa siku. Kabati nilitengeneza Tsh 200,000. Jiko 40,000 Ndo nimewagawa maeneo matano. Kwa siku nakusanya 100,000.

Hata kama umeajiriwa hii ndo fursa iliyopo kwa sasa hapa mjini, achana na biashara kubwa kubwa.
 
Inategemeana na mahali ulipo. Kuna sehemu wakiona umeanzisha biashara ya chips kila mtu kwenye huo mtaa nae anaanzisha biashara hiyo hiyo. Wabongo wengi hawana mawazo mapya. Wanasubiri ulianzishe ili wao waige.
Kwahiyo wewe unashauri watu wasianzishe hiyo biashara Kwasababu watu wengine wata waiga???
Mkuu fikiria tena!
 
Mimi nakupa like mkuu!

Kwenye masuala ya biashara ni ubunifu tu ndio unatakiwa! Kuna watu humu kila siku wanaimba nyimbo za kukosa mtaji lakini ukiwahesabia hela wanayo nywea bia kwa mwezi ni zaidi ya laki!

Nimegundua tatizo kubwa sio mtaji, ni akili! Mimi nafanya hiyo biashara pia, ila mimi nimefungua migahawa nikakabidhi wamama lishe ambao kila mmoja ananikabidhi Tshs 30,000 kila siku!
 
Angalia sehemu ulipo kuna fulsa gani.. Zitumie.. Kila kitu kinaanza na moja
 
Niliambiwa mashine ya kukamulia juisi ya muwa ni sh laki 8 hadi 1.2 M. Kwa mtaji huo inakuwa ngumu kidogo. Zile mashine SIDO ni shillingi ngapi?
 
Hata mm niliulizia ile mashine ya kukamua miwa ya kutumia umeme nikaambiwa 2M. Sujajua zile za kutumia nguvu ya mkono bei yake ipoje
 
Mimi last week nimefanya savei kkoo...kupangisha kisehemu wanatoza elfu 10 kwa siku alafu wanataka kodi ya mwaka...nilichoka na mtaji wangu wa laki5...

Mkuu kesendi kama upo dar wewe upo pande zipi hizo wanazochukua kwa siku?
 
Wanabodi na vijana wenzangu.

Kama huna ajira fanya yafuatayo na uchukue hatua;

1. Tafuta Tsh 200,000 tu.
2. Tafuta eneo la kuchoma viazi/chips hasa karibu na vyuo, msongamano wa watu.
3. Fungua hii biashara ya kuuza chips usione aibu wala kuogopa.
4. Jipe mwaka mmoja tu. Utakuja kuniambia.

Kama hiyo haitoshi, kuna fursa ya kuuza Juice ya Miwa. Nenda SIDO chukua mashine ya kusaga juisi ya miwa tafuta eneo lenye mkusanyiko wa watu nunua grass zako 10 na Ki-meza.

Ukithubutu Tanzania hakuna umaskini, ukiona unaogopa tafuta kijana mpe mtaji msimamie tafuta mkopo wa Tsh 400,000 kwa biashara ya kuuza JUISI YA MIWA. Ni biashara ambayo haina usumbufu wa TIN NO, LESENI YA BIASHARA, WALA KODI YA FREMU.

Mimi binafsi nimeajiri vijana wanachoma viazi/chips na kunipa 20000 kwa siku kama maeneo matano. Mtaji nilianza nao kwa kila kijana 150,000 kodi ya kieneo kwa madalali 1000 kwa siku. Kabati nilitengeneza Tsh 200,000. Jiko 40,000 Ndo nimewagawa maeneo matano. Kwa siku nakusanya 100,000.

Hata kama umeajiriwa hii ndo fursa iliyopo kwa sasa hapa mjini, achana na biashara kubwa kubwa.
Uzi mzuri sana huu, bila shaka uki-combine juice ya miwa na chipsi nzuri hapo hapo unaweza ukafurahia
 
Labda kama zimepanda kutokana na uhitaji lakini wakati naaanza mwaka jana zilikuwa poa
 
Bei ya mashine za kukamulia juice za SIDO ni bei gani?
 
Mimi last week nimefanya savei kkoo...kupangisha kisehemu wanatoza elfu 10 kwa siku alafu wanataka kodi ya mwaka...nilichoka na mtaji wangu wa laki5...

Mkuu kesendi kama upo dar wewe upo pande zipi hizo wanazochukua kwa siku?

Akueleze ili mpe upinzani? Ngoo..huambiwi kamwe hapo hadharani...
 
Biashara ya juice ya miwa IPO poa sana ila ukipata mtaji tu wa machine mambo yote yanakua sawa Mimi sina mtaji wa mashine ila ningepata ningechangamkia hiyo fursa maana maeneo ni mengi sana ya kufanya hiyo biashara
 
Back
Top Bottom