Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Kwa matamshi na mienendo ya kijana mwenzetu Humphrey Polepole katika wadhifa wake mpya kama Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala kwa miaka 56 mfululizo ya uhuru (CCM), Ndg PolePole anazidi kudhihirisha kwamba hakijui Chama Cha Mapinduzi, hasa historia yake ya kumkomboa mwananchi. Ni muhimu akaelewa kwamba Chama hiki cha CCM kilishindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi hata kabla Mwalimu Nyerere hajang'atuka madarakani 1985. Akina Pole Pole na wenzake Lumumba wanajaribu kupotosha ukweli huu na badala yake kuaminisha umma kwamba CCM ilipotea njia baada ya mwalimu kuondoka; kwamba CCM iliachana na misingi yake baada ya Mwalimu kuondoka. Hii sio kweli. Tutaeleza ukweli ambao ni pamoja na kwamba:
1. Misingi ya CCM ambayo Pole Pole et al wanaambia umma kwamba ni lazima irejewe, msingi hiyo hiyo ndio chanzo cha umaskini wa taifa letu.
2. Misingi hiyo ndio ilipelekea CCM kupoteza dira. Ujamaa ilikuwa ni itikadi ya kuunga unga tu (tutaona kwa kifupi baadae). Material basis ya itikadi hii ilitokana na uwepo wa maskini ambapo karibia 90% ya nchi ilikuwa ni rural on the eve of independence. These conditions provided excellent and perfect material and social basis for various petty bourgeois ideology, Ujamaa in particular ambapo ilikuwa ni rahisi kuwaunganisha 90% ya watanganyika weusi kuwa kitu kimoja. Kwa kifupi, Ujamaa as an ideology was an idealization of the life situation of the peasants as well as rationalization of the poor peasants, who constituted almost 90% of the population at eve of independence. Baadae tutakuja kuona kwa undani jinsi gani TANU (bila hata uwepo wa upinzani) ilivunja matumaini ya wananchi ndani ya miaka kumi tu ya azimio la arusha.
3. Misingi hiyo ambayo Pole Pole ameapa kuisimamia, ikirejewa nyakati hizi itatuangamiza kama taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Misingi husika (katika muktadha wa ujamaa) haipo supported by any explicit social theory, ndio maana ilifeli. Itikadi ya Ujamaa ilikuwa ni mkusanyiko tu wa glorious description of the past (very flawed description historical wise). Itikadi ya ujamaa was definitely a very powerful statement of an idealist policy (Mwalimu wa essentially an idealist more than anything), lakini itikadi hii haikuwa na political programme. Ujamaa ulikuwa na maono makubwa ya mbeleni (grandiose vision of the future), lakini it lacked ground theory of society. Ndio maana katika yote, legacy pekee ya Mwalimu Nyerere itakayobakia pengine milele ni kwamba - he had very sincere objectives/alikuwa na Nia ya dhati' kuona taifa lake linasonga mbele. Na inaishia hapo kwa sababu mijadala mingine itakuwa clouded na mapungufu ya utawala wake, ambayo yanaendelea kututafuna hadi leo na yataendelea kututafuna iwapo kweli PolePole na wenzake Lumumba wataamua kurudi katika misingi husika.
Ni muhimu sana PolePole akaelewa kwamba hata wakati wa urais wa Mwalimu Nyerere, TANU/CCM haikuishi hata siku moja katika ujamaa na kujitegemea. Kwa mfano, Ujamaa ulitegemea Ubepari on a daily basis. Misingi ya kuhalalisha itikadi ya ujamaa kwa mfano huduma bure za kijamii na juhudi za maendeleo kwa mfano kupitia import substitution industries, yote haya yalitegemea moja kwa moja mifuko ya mabepari - kwa maana ya AID & Foreign Direct Investment. Ilikuwa ni contradiction kubwa sana ambayo ilipita unnoticed! Tutaona hili kwa undani baadae.
Mafanikio (kama sio matumaini ya mafanikio) ya TANU yalikuwa ni ya muda mfupi sana - 1967-1977. Baada ya hapo, TANU iliyoimbwa kwamba 'yajenga nchi' ikaanza kuyumbisha na hatimaye kubomoa nchi. Na haya yote yaliyokea wakati wa mfumo wa chama kimoja, hasa kuanzia miaka ya kati ya sabini kuelekea miaka ya themanini. Hadi leo, wasiwasi juu ya 'amani na utulivu' wa nchi unatokana na matatizo ya CCM yenyewe (ndani ya CCM), sio nje ya CCM. Nje ya CCM kuna mbadala wa mfumo huu unaoendelea kuangamiza taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa (hasa demokrasia).
Ni bahati mbaya sana mapambano dhidi ya mfumo huu mbovu yanageuzwa na akina Pole Pole na wenzake pale Lumumba kuonekana kwamba ni mikakati ya upinzani/ukawa dhidi ya tunu za amani na utulivu. Ni ajabu sana kwa mtu eloquent kama polepole kuwa consumed na ulaghai kama huu.
Wengine tulishaondoka CCM muda mrefu hasa baada ya kuelewa ukweli wote hapo juu. Tumeamua kujitenga na uongo. Kuendelea kubakia CCM ni kuendelea kulea ujinga, jambo ambalo ni mmoja wa maadui watatu wa maendeleo ambao CCM hiyo hiyo ikiwa TANU iliwatambua mara tu baada ya uhuru. The fact kwamba maadui hao wanaendelea kutuzonga miaka karibia sitini baada ya uhuru ni kielezo tosha kwamba linapokuja suala la maendeleo ya wananchi, CCM imeishiwa pumzi.
Treating CCM synonymously as the STATE na kuaminisha wananchi wasio na uelewa kwamba the two are inseparable ndio nguzo kuu inayoipa CCM mileage, ndio inayojenga uhalali wa kufanya maovu yake yote na kutumia mabavu kuhalalisha kuziba midomo wapinzani, kuangamiza demokrasia, kunyima vyombo vya habari uhuru nk. Jitiada zote hizo ni kuzuia wananchi wasielewe ukweli ambao nimeugusia kidogo hapo juu.
Binafsi nafurahi sana kwamba hatimaye kijana wa generation yetu/kizazi chetu ambae ni mwelewa zaidi ya aliyemtangulia, amepata nafasi ya kukitumikia chama (CCM) katika nafasi hiyo ya itikadi na uenezi. Tutakabiliana na PolePole kwa hoja, na atatuelewa tu, na pengine atakuja chukua maamuzi magumu kuliko haya ya juzi ya kutamka wazi kwamba mfumo sahihi ni mfumo wa serikali tatu. Na hii sio mara ya kwanza kwa polepole kuunga mkono hoja zangu, kwani alishafanya hivyo wakati wa mjadala wa serikali tatu wakati ule bunge la katiba likiketi - rejea:
.
Matamshi kama haya kwa kawaida huwa ni karibia na usaliti ndani ya chama kama sio uhaini. The fact kwamba anaendelea kubakia katika nafasi yake ya uongozi CCM huku akiwa hana imani na sera kuu ya CCM (mfumo wa serikali mbili) ni kielelezo tosha kwamba something is brewing. Nimalizie kwa kusema kwamba ni muhimu kwa Ndg Pole Pole akatambua kwamba mfumo wa serikali mbili ni moja ya nguzo kuu tatu zilizokipa CCM uhalali wa kisiasa nchini. Nguzo nyingine mbili zilikuwa ni Mfumo wa Chama Dola na Itikadi ya Ujamaa. Kufikia hapa, kwa wanaoelewa wataona wazi kwamba nguzo zote hizi tatu zimemomonyoka, na ndio maana Chama hiki kina struggle kujitafutia uhalali nje ya sanduku la kura, huku kijana mwenzetu PolePole akiamua kuungana na juhudi hizo. Hawezi kufanikiwa na historia itakuja kumuandika hivyo.
Itaendelea…