Humphrey Polepole, unahitaji kuelimishwa kuhusu CCM

Humphrey Polepole, unahitaji kuelimishwa kuhusu CCM

Mie niliacha kumsikiliza huyu jamaa au kusoma chochote kinachotoka kinywani mwake baada ya kugundua kwamba hajitambui kwa kukubali kile kile ambacho alikuwa akikipinga.
Ila unaendelea kumsikiliza Mbowe na lowasa, vichekesho
 
kwahiyo Pole pole anataka kutuaminisha kuwa ccm itabadirika na kuleta maendeleo?

Pole pole ile mifumo uliyokuwa unaiponda kipindi kile cha kudai katiba ya warioba vp umeitupilia wapi?
 
Mie niliacha kumsikiliza huyu jamaa au kusoma chochote kinachotoka kinywani mwake baada ya kugundua kwamba hajitambui kwa kukubali kile kile ambacho alikuwa akikipinga.
Mkuu hawa watu ni wazuri sana wa kuongea, wakiachwa umma utapotoka. Ndiyo maana tupo hapa kumuonyesha jinsi alivyokengeuka

Sina tatizo akieleza sera za chama kama katibu mwenezi. Hiyo ndiyo kazi yake ya mkate wa kila uchao

Ninatatizo anapoamua kuufanya umma wote kama ni CCM na wana haki ya kutuamulia hatma yetu

1. Humphrey anasema, serikali na chama wamepata malalamiko ya wananchi kuhusu 'kuzurura' kwa viongozi. Hivyo wameamua viongozi wakae maeneo yao kuhamasisha maendeleo

-HP alikuwa mjumbe wa tume ya katiba, sina shaka anaelewa katiba imetoa uwezo wa wananchi kuwachagua viongozi wao ambao ni wabunge na kuwakataa muda ukifika

Si kazi ya HP na CCM kuamua nini wabunge wanafanya, NI kazi yake kuamualia wabunge wa CCM wanapaswa kufanya nini. Amri hiyo anayoipigia debe ni ya wanaCCM si wananchi wote

-HP anafahamu haki ya kufanya mikusanyiko popote nchini ni ya kikatiba kwa wananchi na kisheria kwa vyama kama ilivyoanishwa katia sheria za msajili wa vyama.

Mjumbe wa tume ya katiba anaposhindwa kuelewa hili, inasikitisha sana.

Mbaya zaidi angekaa kimya haijambo, anapigia debe jambo analojua si la haki wakati alikuwa mjumbe wa kutuandikia utaratibu wa haki zetu yaani katiba. Hili ni tatizo kubwa na jambo la hatari sana

2. HP anasema wananchi wanataka rushwa, ufisadi na ubadhirifu uondolewe.Hana source ya wananchi gani. Wanachama wa CCM si wananchi wote hivyo takwimu hana anababisha

3. Anasema serikali ipige rushwa huo ni msimamo wa CCM na irudi kwa wanaCCM wanyonge.

Atarudishaje chama kwa wanyonge, ikiwa wenyechama wanakutana Dodoma na kugawana milioni 10?

Kurudisha chama ni kununua kofia na t-shirt kwa wanyonge wao wakilamba 10M kwa siri

4. HP anasema wananchi wamewapa mandate ya kutawala.
Hili linanitumbusha kauli yake ya kwamba Jecha alipaswa kufuta matokeo kwasababu ni 'symbol' ya tume. Mjumbe wa tume ya katiba anayosema ni ya wananchi lakini hajui nini maana ya tume

5. HP anasema katiba imeahirishwa ili wananchi waongee lugha moja.
Miaka 3 iliyopita HP alikuwa busy katika mikutano nchini (ambayo sasa anaita kuzurura) akipiga kampeni ya katiba

Katika 'uzururaji' huo alikutana na kipigo cha kada Makonda pale Ubungo.

HP alilaani tukio hili kama kuvunja haki za katiba na za wananchi kuongea na kukusanyika.

Leo anatuambia viongozi wasifanye siasa wahamasishe maendeleo akiwaita wazururaji

6. Lugha ya katiba haina shida, anapaswa kumwambia kada Makonda lugha ya katiba ni maongezi, si viti na makonde. Wapi alipata hoja ya lugha ya katiba? Wapi duniani kuna lugha ya kuandika katiba.

7. HP anatoa namba ya simu mwenye shida ampigie. Hivi huyu ana nafasi gani katika serikali?
Tazama 'kilevi' cha madaraka kinavyoweza kuhadaa umma. HP ni nani katika serikali hii

Huyu ni mjumbe wa tume ya katiba asiyeweza kuelewa mipaka ya chama na serikali

Haya ni machache kadri tunavyosonga tutaeleza jinsi gani viongozi wa nchi hii yenye rasilimali na umasikini walivyoitia umasikini kwa miaka 50.

Umasikini wa miaka 50 haukuanza na wazee, ulianza na vijana kwa uongo na unafiki, leo ni wazee. Hawakuzaliwa katika nafsi hizo, wamekua nazo na kuzifanya tabia zinazokubalika katika jamii

Kama hatuwezi kukemea tataendelea kuwa masikini miaka 50 mingine.

Si bahati mbaya ni watu wanaofanya uongo kuwa sehemu ya maisha kama alivyowahi kutueleza HP
 
Back
Top Bottom