Humphrey Polepole unaamaanisha nini kusema hivi?

Humphrey Polepole unaamaanisha nini kusema hivi?

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,591
Reaction score
31,128
Nawasalimu kwa jina la Tanzania

Polepole amenukuliwa akisema kuwa katika awamu ya Tano aloondoka ni mtu mmoja tu MAGUFULI , lkn serikali ni ileile ,chama ni kilekile

hivyo hakuna awamu ya sita ,Tusiwe tunachanganya.

SWALI?
Wataalam humu ndani naombeni nielemishwe "kwa hiyo anachosema POLEPOLE ni sahihi " kwamba hii serikali anayoongoza mama ni ya Awamu ya Tano na si ya Sita na tumhesabie awamu ya sita 2025?

Na je?

Ikitokea Mama asigombee awamu ya 2025 awamu ya tano itahesabika imetawala kwa miaka 10 ( vipindi vyote viwili)

Kwa unyenyekevu naomba kuelimishwa maana kipindi hiki Tunachanganywa sana jmn!!! kila mtu ana lake jambo tunashindwa kujua which is which.

karibuni !
JamiiForums1627645906.jpg
 
Ni awamu ya sita kwa sababu kipindi cha pili awamu ya tano hakikufikia nusu ya muda wake kwa hiyo hakina sifa ya kuitwa awamu kwa maana hiyo Rais aliyepo kaanza awamu ingine ya sita
 
... naona wanajaribu kumrudisha Samia "kwenye mstari" ili aweze kurithi mauchafu ya mtangulizi wake maana hata yeye (Samia) alikuwepo halafu jana akadai eti yeye "anaangushiwa jumba bovu" utadhani hakuwa sehemu ya serikali iliyopita! Sasa Polepole na genge lao wameamua kuchukua hatua; na hatua ya kwanza ni "kumrudisha kwenye mstari" kwamba hii bado ni Awamu ya Tano. Then mengine yatafuata.

Wameshtuka Mama anataka "kuchomoa kiaina" kuharibu legacy ya "kipenzi chao" and therefore hatma ya genge pia itakuwa shakani endapo Samia "atasimama na wananchi" kama alivyodai kwenye hotuba yake jana. Kauli ya Polepole si yake; bali yeye ni kipaza sauti tu; mtambo uko nyuma huko!
 
Itaitwaje awamu ya 6 wakati hakuna uchaguzi

uliofanyika!?……………

Wabunge ni wale wale, speaker ni yule yule…….

Waziri Mkuu ni yule yule…..

Hakuna awamu ya 6 hapa acheni unaa…….

Pole pole yuko sahihi kabisa……..
 
Hiyo statement ni ya "wenye nchi" na si ya polepole. I know these people. They're very very smart. Mama awe makini tu.
Unaongea mambo shallow lakini yana mantiki.
nakumbuka uzi wako mmoja daah naishia. kushangaa ulivyoandika na ku flow ikaja. kutokea vile vile
 
Ni sehemu tu ya kujitoa ufahamu, kweli viongozi wakuu wale wale, ila mitizamo imebadilika sana juu ya kuendesha nchi na utendaji ndani ya serikali hata diplomasia ya kimataifa, ona jinsi mahusiano ya kimataifa na mashirika yake, mahusiano ya tra na wafanyabiashara, kupotea watu, kuweka ndani watu kulikofanywa na ma DC, hata lugha sasa ujatambua kuwa kuna washirika wa maendeleo sio mabeberu tena.

Kwa hiyo uwezi sema hawamu hizi hazina tofauti, ingawa zote zinatekeleza ilani ya chama tawala. Polepole anakuwa mbabaishaji sijui kwa nini iliudhuria kipindi star TV, wakati hakuwa tayari kujibu maswali, na hofu yake kuwa akijibu ipaswavyo uenda akawaudhi wakubwa wake! Asinge enda.
 
Nawasalimu kwa jina la Tanzania

Polepole amenukuliwa akisema kuwa katika awamu ya Tano aloondoka ni mtu mmoja tu MAGUFULI , lkn serikali ni ileile ,chama ni kilekile

hivyo hakuna awamu ya sita ,Tusiwe tunachanganya.

SWALI?
Wataalum humu ndani naombeni nielemishwe "kwahyo anachosema POLEPOLE ni sahihi " kwamba hii serikali anayoongoza mama ni ya Awamu ya Tano na si ya Sita na tumhesabia awamu ya sita 2025??

Na je?

ikitokea Mama asigombee awamu ya 2025 awamu ya tano itahesabika imetawala kwa miaka 10 ( vipindi vyote viwili)



kwa unyenyekevu naomba kuelimishwa maana kipindi hiki Tunachanganywa sana jmn!!! kila mtu ana lake jambo tunashindwa kujua which is which.

karibuni !
View attachment 2033387
Na ilani ni ile ile!
 
Itaitwaje awamu ya 6 wakati hakuna uchaguzi

uliofanyika!?……………

Wabunge ni wale wale, speaker ni yule yule…….

Waziri Mkuu ni yule yule…..

Hakuna awamu ya 6 hapa acheni unaa…….

Pole pole yuko sahihi kabisa……..
... kwani determinant ya awamu ni uchaguzi? Sheria ya Awamu inasemaje (kama ipo)?
 
Ni upuuzi mkubwa kubishania awamu.
Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21 alitawala kwa awamu ngapi?
Kama awamu ni nongwa sana tubaki na maneno Rais wa sita tu, basi.
 
Mlio karibu na Pole pole mshaurini akubaliane na ukweli kuwa zama zimebadilika na hivyo akae kimya sasa anapoelekea watu wataanza kumpuuza.
 
Back
Top Bottom