Humphrey Polepole: Salamu Zangu Kwako

Humphrey Polepole: Salamu Zangu Kwako

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,425
Reaction score
3,300
1408170205993.jpg
HUMPHREY POLEPOLE:Salamu zangu
za Mwisho wa Wiki kwenu:
1. Nilipata fursa ya kuwapitisha wanachama 180 wa Jukwaa la Katiba katika Rasimu ya Katiba Toleo la Pili. Nikazungumza nao pia juu ya wajibu wa Asasi za Kiraia kudai mchakato huu ukamilike kwa mafanikio kama ilivyokusudiwa na waliopewa dhamana wakati huu kuheshimu maoni ya wananchi. Nchi hii ni zaidi sana ya maslahi yetu binafsi na makundi

2. Nimemaliza kuandika Makala yangu itakayotoka Gazeti la Mwananchi Jumapili Agosti 17. Jumapili hii nimezungumzia juu ya Uraia Pacha, nimeeleza changamoto zake na nimeweka suluhisho linalopendekezwa na Rasimu ya Katiba.

3. Nimepokea Mualiko kutoka Gazeti la Rai linalotoka kila Alhamisi kwamba niwe natoa Maarifa huko uandishi wa Makala. Nimekubali. Na sasa mtaanza kunisoma katika gazeti la Rai kuanzia wiki ijayo Alhamisi Agosti 21.

4. Nitawajulisha hivi punde vipindi vya Televisheni nitakavyokuwa nikitoa elimu kwa umma wiki ijayo ili twende pamoja. Niwatakie Mapumziko mema ya Wikendi. Usisahau kusoma magazeti, kusikiliza redio na kuangalia Televisheni ili uendelee kupata ufahamu wa nini kinaendelea katika Mchakato wa Katiba Mpya. Hatma ya kupatikana kwa Katiba Mpya iko Mikononi Mwako.

Asante na Tafakari
 
Mkuu eneza elimu wagumu wa mioyo wakuelewe
 
Nadhan hili litamkera yule Mjumbe wa Bunge la Katiba alosema wajumbe wa tume wasitoe maoni tena kuhusu mchakato wa katiba,na yule mwenyekit alosema kuwa ITV(HAKUITAJA) iangaliwe
 
Akiona mzee san'gweli haya maneno weeknd yake inaharibika kabisa........mijadala ya katiba ni muhimu sana kwa uhai wa katiba bora,asante sana pole pole
 
Wangepatikana Vijana Wazalendo kama hawa pindi tunapopata fursa ya kuwa mbele kuitetea nchi dhidi ya Mchwa hatari inapendeza sana.
 
Cc >>>> Msalani, mwanadiwani, utaifakwanza, mmaramguoriginal, Mandla Jr, Na Team Buk 7
Tunaomba mawazo yenu.
 
View attachment 177860
HUMPHREY POLEPOLE:Salamu zangu
za Mwisho wa Wiki kwenu:
1. Nilipata fursa ya kuwapitisha wanachama 180 wa Jukwaa la Katiba katika Rasimu ya Katiba Toleo la Pili. Nikazungumza nao pia juu ya wajibu wa Asasi za Kiraia kudai mchakato huu ukamilike kwa mafanikio kama ilivyokusudiwa na waliopewa dhamana wakati huu kuheshimu maoni ya wananchi. Nchi hii ni zaidi sana ya maslahi yetu binafsi na makundi

2. Nimemaliza kuandika Makala yangu itakayotoka Gazeti la Mwananchi Jumapili Agosti 17. Jumapili hii nimezungumzia juu ya Uraia Pacha, nimeeleza changamoto zake na nimeweka suluhisho linalopendekezwa na Rasimu ya Katiba.

3. Nimepokea Mualiko kutoka Gazeti la Rai linalotoka kila Alhamisi kwamba niwe natoa Maarifa huko uandishi wa Makala. Nimekubali. Na sasa mtaanza kunisoma katika gazeti la Rai kuanzia wiki ijayo Alhamisi Agosti 21.

4. Nitawajulisha hivi punde vipindi vya Televisheni nitakavyokuwa nikitoa elimu kwa umma wiki ijayo ili twende pamoja. Niwatakie Mapumziko mema ya Wikendi. Usisahau kusoma magazeti, kusikiliza redio na kuangalia Televisheni ili uendelee kupata ufahamu wa nini kinaendelea katika Mchakato wa Katiba Mpya. Hatma ya kupatikana kwa Katiba Mpya iko Mikononi Mwako.

Asante na Tafakari

Go go go Humphrey; sema usiogope sema; umma una hamu nakiu kubwa ya kujua nini chanzo cha mtafaruku huu kuhusu mchakato wa katiba mpya; umma unataka kuelimishwa.
Kuvunjwa kwa tume ya mabadiliko ya katiba na kufungwa kwa tovuti yake hakuwanyimi wajumbe wa tume hiyo haki yenu ya kiraia kutoa upande wenu wa sakata hilo.

Go Humphrey Go.
 
Ndo wakati wa Wajumbe kujitetea na kuelimisha panapokosewa.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Yes Mr Pole Pole......uko sahihi....but niseme kumbe ujinga huu wa watz wengi ni furaha kwa watu,wajumbe wa bunge la katiba hasa wa ccm,201 na wale wanapinga rasimu hawataki mtu yeyote,tasisi au chombo chochote cha habari kutoa elimu kuhusu rasimu ya katiba!hii nimeshangaa sana!.But watu hawa sio wa kesho hivyo ni vyema wakajua kuweka vitu vya kufikikan kwenye katiba kama jinsi tunavyoona ni hatari kwa nchi.Wajumbe lazima waelewe na washtuke mbona watanganyika wanadai sana mamlaka?.Mimi ni waambie tu tumeshawatambua wote,na wajue ipo siku ardhi hii itapata mamlaka yake...hawasomi alama za nyakati,Tanzania ni muungano tu na nje ya muungano hakuna kitu kama hicho.Siasa za kibepari inaingia na kila mtanganyika anaanza kuangalia yeye atamiliki nini juu ya ardhi hii,sasa watu wasio na uelewa wanadhani watavumilia!.Rudini ktk rasimu na mheshimu maoni ya wananchi.
 
Asanteeeeeeee, mpaka wajinyonge safari hii....Ni mwendo wa kukaza kamba shingoni mwao mpaka wapate asyphyxia.
 
Ndugu Polepole tupo pamoja na Mungu hawe nawe siku zote. Kwani bila kujitoa, Taifa hili litakwama. Vijana inabidi tusiangalie ubinafsi wetu bali tupiganie nchi yetu kwa niaba ya wanyonge.
 
You are charismatic,I adore you Polepole.keep it up,the road ahead of you is paved.
 
Back
Top Bottom