Humphrey Polepole: Salamu Zangu Kwako

Humphrey Polepole: Salamu Zangu Kwako

Good move Humphrey All the best comrade.
 
Bw. Polepole nakupongeza sana kwa darasa murua unalotupatia sisi Watanzania wenye muelekeo wa kupenda nchi yetu kuhusu Rasimu ya Katiba. Usikatishwe tamaa na manyang'au wanaotaka kujilimbikizia kila kitu. Ukombozi wako naufananisha na Edwardo Mondlane,Samora Machel,Augustono Neto na Nelson Mandela ambao walifungwa kwa ajili ya ukombozi wa nchi zao.Bravo Polepole.Aluta continua!
 
Vijana wezangu tuigeni mfano dhairi kutoka kwa POLEPOLE,wa kusimamia maslahi ya umma!
 
H.Polepole ni mzalendo aliyejitambua, mwenye kuangalia maslahi mapana ya nchi yetu, Mungu akulinde dhidi ya mahayawani
 
NOTE:kipindi hiki usikubali ofa yoyote ya kukata kiu mahala kama Leaders hata toka kwa rafiki yako,bado tunakupenda bro wewe ni mwiba kwa wale wanaotaka kuibinya rasimu ya pili.Bado yule mpare aliyepongezwa kipindi kile tuna msiba mzito yupo!!!ni hayo tu.
 
Kijamaa kibishi hiki! Jamani Li-Sitta si limesema vipigwe marafuku hivi vipindi vya kuwaamsha wa-Tz kuhusu katiba mpya? HP, TL, JJM, DK, MM, FAM, HJM, JMBATIA, ZZK (ingawa kalegeza makalio), hii ndo ilikuwa timu yangu ya ushindi! Vijana nyie ndo mnatuangusha!! Magamba huwa hayapumui!!
 
Muheshimiwa polepole shukrani!na pole pole watatii tunachotaka wa-Tanzania
 
Pole pole aliagizwa kuwasikikiza wananchi wanasema nini/wanataka kitu gani na aliwasikiliza na akaenenda kama alivyoagizwa ,jitahidi sana kuchukua tahadhari katika njia zako sababu umeonekana wewe unasema bila kuogopa na ni vizuri sababu tumeshuhudia kwa Marehemu Daudi Mwangosi tumeona kwa Ulimboka tumeona Saed Kubenenea na wengine wengi.
 
tupe contact mkuu ,na sisi huku tunaelimisha vijana na baadhi ya vipengele huwa ni shida
 
Pamoja na ifweero, m...vi yatagonga pichu zao na kugeuza
 
Kijana mwenzangu nakuheshimu sana kaka...... taifa linavurugwa na walafi
 
View attachment 177860
HUMPHREY POLEPOLE:Salamu zangu
za Mwisho wa Wiki kwenu:
1. Nilipata fursa ya kuwapitisha wanachama 180 wa Jukwaa la Katiba katika Rasimu ya Katiba Toleo la Pili. Nikazungumza nao pia juu ya wajibu wa Asasi za Kiraia kudai mchakato huu ukamilike kwa mafanikio kama ilivyokusudiwa na waliopewa dhamana wakati huu kuheshimu maoni ya wananchi. Nchi hii ni zaidi sana ya maslahi yetu binafsi na makundi

2. Nimemaliza kuandika Makala yangu itakayotoka Gazeti la Mwananchi Jumapili Agosti 17. Jumapili hii nimezungumzia juu ya Uraia Pacha, nimeeleza changamoto zake na nimeweka suluhisho linalopendekezwa na Rasimu ya Katiba.

3. Nimepokea Mualiko kutoka Gazeti la Rai linalotoka kila Alhamisi kwamba niwe natoa Maarifa huko uandishi wa Makala. Nimekubali. Na sasa mtaanza kunisoma katika gazeti la Rai kuanzia wiki ijayo Alhamisi Agosti 21.

4. Nitawajulisha hivi punde vipindi vya Televisheni nitakavyokuwa nikitoa elimu kwa umma wiki ijayo ili twende pamoja. Niwatakie Mapumziko mema ya Wikendi. Usisahau kusoma magazeti, kusikiliza redio na kuangalia Televisheni ili uendelee kupata ufahamu wa nini kinaendelea katika Mchakato wa Katiba Mpya. Hatma ya kupatikana kwa Katiba Mpya iko Mikononi Mwako.

Asante na Tafakari

Kaka usitupeleke RAI lilishakuwa gazeti la udaku.Tupeleke -----,ngo gazeti linalosomwa na watu wanaotafuta maarifa.
 
TV yenu UKAWA inajulikana ni ITV huna sababu ya kutuambia, tunajua
 
Bw. Polepole nakupongeza sana kwa darasa murua unalotupatia sisi Watanzania wenye muelekeo wa kupenda nchi yetu kuhusu Rasimu ya Katiba. Usikatishwe tamaa na manyang'au wanaotaka kujilimbikizia kila kitu. Ukombozi wako naufananisha na Edwardo Mondlane,Samora Machel,Augustono Neto na Nelson Mandela ambao walifungwa kwa ajili ya ukombozi wa nchi zao.Bravo Polepole.Aluta continua!

unampongeza mtu ambaye amenunuliwa kwa pesa kiduchu kweli kukiuka kiapo alichokula wakati anaapishwa kuwa mjumbe wa tume ya WARYOBA cha kutojiingiza kwenye siasa? huyu hana tofauti na YUDA
 
Vijana wezangu tuigeni mfano dhairi kutoka kwa POLEPOLE,wa kusimamia maslahi ya umma!

Pole pole anasumbuliwa na njaa tu, hana lolote la kuiga kutoka kwake, labda kama na wewe una njaa kama yeye utafuta nyao zake.
 
Back
Top Bottom