Humphrey Polepole njoo unijibu haya maswali kuhusu CCM yako

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Baada ya kuona umepewa uenezi na CCM naona umekomaa sana sana kutetea chama chako as if hujui kila jambo lolote baya linalotokea wa kulaumiwa ni nyie CCM sio wapinzani!! naomba sasa kwa heshima yako uje unijibu haya maswali na unipe ufafanuzi wa kutosha

1. Kusitishwa kwa nyongeza za mishahara na ajira na kupanda vyeo kwa watumishi wa uma nani alaumiwe kati ya CCM na upinzani?

2. Kupanda kwa makato kwa watumishi waliokopa loan board kwa ghafla kutoka 8% hadi 15% nani alaumiwe kati ya CCM na upinzani?

3. Ikitokea watu wakafa kwa njaa katika kipindi hiki ambacho mnajaribu kukanusha kuwa hakuna njaa.. je nani alaumiwe kati ya CCM na Upinzani?

4. Kusitisha kuonyesha bunge live, ninyi kama CCM mmenufaika na nini na upinzani umekosa nini?

5. Kushindwa kusambaza zile mil 50 kila kijiji hili pia tuwalaumu wapinzani kwa kukwamisha?

6. Kushuka kwa thamani ya shilingi hili pia wapinzani wanahusika?

Najua utanijibu bila shaka, asante sana baada ya hapo nitaweka maswali ya nyongeza.

Allan

allanclement6@gmail.com
 
3. Ikitokea watu wakafa kwa njaa katika kipindi hiki ambacho mnajaribu kukanusha kuwa hakuna njaa.. je nani alaumiwe kati ya CCM na Upinzani?
Kama watakufa wanaCCM nyie wapinzani inawahusu nini? Sisi tutazikana.
 
Polepole anaelekea kule kule kwa Nape.yaani hana la kusema zaidi ya kusubiria matamko ya wapinzani
CCM jinga la fikra lakini sasa inasadiwa na mzee wa Kuropoka
Sitashangaa Kabudi akaanza kuropoka kama Bulembo yule wa darasa la saba
 
Back
Top Bottom