Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,914
- 3,959
Kumekuwa na tabia ya ajabu sana miaka ya hivi karibuni, yaani mtu akiwa tu na nafasi na kupewa "microphone" anajiona kama sijui yupo chini ya mwamvuli gani, wanajisahau kuwa CCM inawajibika kwa wananchi na badala yake wanawaona wananchi kama watumishi wa CCM.
Kila taasisi, chama, kikundi au umoja una siri zake zinazotawala uwepo wake na siri hizo hata kama zinafahamika hazipaswi kuwekwa wazi kwa kila mtu mathalani kauli ya Mheshimiwa fulani kuwa "matokeo ya kura siyo lazima yawe ya kwenye boksi, inategemea nani anahesabu na kutangaza"...ni miongoni mwa kauli zinazowakatisha tamaa sana wapiga kura, mtu anajiuliza kama anayehesabu na anayetangaza ana uwezo wa kuwachagulia wananchi Kiongozi ni ipi nguvu au sauti ya mpiga kura?. Kauli za hivi ni kauli zisizofaa kabisa kutamkwa mbele ya halaiki ya wanachi hata kama wanaoonekana ni wajinga kiasi gani.
Si hivyo tu ipo kauli nyingine ya hivi karibuni ambayo kwa kweli inaonesha kuwa siyo kila mwanachama hata kama ni kiongozi anapaswa kukisemea chama . Kiongozi kweli unatamka kuwa "............mazingira ya 2020 ya madiwani kupita bila kupingwa yalitengenezwa na Serikali" Halafu bila aibu anagusia na mazingira ya ubakwaji wa demokrasia kwa kusema ni Serikali?.
Haya masuala yanaiachia Serikali maswali magumu ambayo yamezalishwa na wanachama waliojikinga chini ya kivuli cha chama kiasi cha kuwaona wenye chama ni kama watumishi wao.
Ipo haja sasa ya kuhakikisha Chama kinapunguza washika microphone.