NITAZUNGUMZA NA UMMA 31 JULAI 2025 SAA 2:00 USIKU
Mungu akipenda Tarehe 31 Julai 2025 siku ya Alhamisi saa 2:00 Usiku nitazungumza na umma na nitashirikisha wanahabari ambao baada ya maelezo yangu awamu ya pili watakuwa na nafasi ya kunihoji maswali mbali mbali kwa kadiri watakavyoona wao inafaa. Mazungumzo haya yatakuwa mubashara (LIVE)Wanahabari watakaoshiriki ni;-
Deodatus Balile
Mtozi Aloyce Nyanda
Kalvin Raphael (Zungu)
Awamu hii pili bado nitakuwa natoa rai kwa CCM kujirudi na kufanya marekebisho ambayo yatafanya Chama kiende kwenye uchaguzi na Mgombea Mpya na kikiwa kimeijenga imara na madhubuti oganaizesheni ya Chama. Mwaka 2025 ni Mwaka wa kuifanya CCM Mpya.
Kwa kiasi nitatoa sababu za msingi za kufanya mabadiliko ya uongozi Mwaka huu na nitaweka ushahidi.
Mungu akawabariki na kuwalinda watu wote wenye dhamira njema na mustakabali wa sasa na kesho wa Nchi na Taifa letu la Tanzania 🇹🇿 namwomba Mungu pia akawape moyo wa nyama wakuu wetu ili waweke mbele maslahi ya Nchi na Taifa letu na sio Maslahi binafsi.
Wenu,
Ndugu Humphrey H. Polepole