Humphrey Polepole: Niliambiwa Rais Samia ameagiza nifukuzwe kazi nikiwa Cuba na mafao yangu yote nisipewe

Humphrey Polepole: Niliambiwa Rais Samia ameagiza nifukuzwe kazi nikiwa Cuba na mafao yangu yote nisipewe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Balozi aliyejiuzulu, Humphrey Polepole, akizungumza kwa njia ya mtandao, Septemba 18, 2025, amesema amesikia kuhusu kuitwa na Jeshi la Polisi lakini bado kuna tatizo Serikalini kwa sababu walipaswa kuihoji Serikali kwanini haijanirejesha nchini baada ya mimi kuondolewa kazini.

Amesema hata alipoajaribu kuuliza watumishi wenzake kuhusu utaratibu wa kurejea nchini kwa Watumishi wanaofanya kazi nje, aliambiwa Rais Samia ameelekeza afukuzwa kazi na stahiki zake zote asipewe.

Amehoji inakuwaje Serikali iliyomtelekeza Cuba inamtaka afike Polisi wakati haikumrejesha nyumbani ikiwa hiyo ni Haki ya Mtumishi.

Vilevile, ameshauri Jeshi la Polisi kufanyia kazi hoja zake badala ya kumtafuta yeye.

 
Haka kajamaa kalishajipanga, na nadhani hayo ni machache kati ya mengi aliyojua lazima yatatokea.
 
Polepole ana mengi ya kuongea sio hizi blaa blaah ngoja tuone baada ya uchaguzi polepole ataongea nini. Hapa ndo mashaka yangu yapo na Polepole msisahau aliyemleta kwenye siasa za bongo
 
Mlijipa matumaini makubwa kuwa jamaa ni jasusi.... 🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom