Humphrey Polepole ana codes

Natamani sana tungepata watu weledi wa kutufungulia 'codes' katika hiyo hatua aliyochukua Polepole ila wapuuzi tu ndio wametangulia kujadili hapo juu! Naitamani sana ile Jamiiforums ya kabla ya 2015! Tulikua na watu humu bwana!
Wewe ambaye sio mpuuzi lete nondo za 20158
 
Sisi mabichwa komwe hata hatuelewi lolote hapa. Tukakojoe tulale.
 
Reactions: Ame
Na wewe tuambie soka,mdude na wengine wengi 84 kama taarifa ya TLS ilivyo sema wako wapi?awamu ya sita imewaficha wapi?
 
Na wewe tuambie soka,mdude na wengine wengi 84 kama taarifa ya TLS ilivyo sema wako wapi?awamu ya sita imewaficha wapi?
Taarifa ile ilisomwa mbele ya Jumanne Muliro ikiwa ni siku chache tu tangu Sativa atekwe.

Sativa aliwekwa live kupitia conference na kutoa maelezo yake ila Muliro akakana sio wao walimteka.

Sasa mtu anawezaje kuvuka checkpoints zote kutoka Dar es Salaam hadi Katavi mbugani na kupigwa risasi kichwani?

Polisi hadi leo hawajatoa ripoti ya uchugnguzi wa tukio hilo , mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama alipoulizwa anajibu no comment.

Soka aliitwa kituoni akafuate pikipiki yake iliyopotea akaingia shaka baada ya kufanya mazungumzo akashauriwa asiende pekeyake aambatane na mwenzie hadi leo wawili wote hawajawahi kuonekana tangu August 28 mwaka jana.

Mdude kavamiwa kwake na watu waliojitambulisha ni polisi wamempiga kavuja damu za kutosha na wameondoka nae leo ni mwezi wa pili sasa hajulikani alipo.

Hapo unataka TLS ndio wafanye majukumu ya inveatigation ilhali wameshatoa majibu na wanaotakiwa kufanya kazi yao wako kimya?

Polisi majuzi wanatoa ripoti eti waliopotea walijiteka , wivu wa mapenzi na visasi , hivi inakuja akilini mtu ajiteke kutoka Dar es Salaam hadi Katavi mbugani?

Njia pekee ni kupata vyombo huru vya uchunguzi na mfumo mpya wa polisi tu na sio hawa polisi ambao ni tawi la CCM.


View: https://www.youtube.com/live/Ve8Du-0fxAo?si=b2eEQixpqaV4lr1z
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…