Humphrey Polepole afunguka, Maaskofu semeni tu

Humphrey Polepole afunguka, Maaskofu semeni tu

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Sifieni kama kuna mambo ya kusifia na onyeni kama kuna mambo ya kuonya lakini hekima busara kwa sababu kauli hiyo ni kauli ya moto inaweza ikatujenga inaweza ikatubomoa.Kuna namna nyingi za kurekebisha, tusije tukageuza na kujadiliana na Maaskofu, Askofu anasema tunamjibu, tutakuwa tunamkosea Mungu.

Mimi sitaki kusema Maaskofu wamekosea au hawajakosea lakini nataka kusema haya majadiliano ukiyaangalia yanatokea wapi? Tusije tukaingia kwenye mtego wa Ibilisi tukajikuta tukimtizama askofu fulani tunaona chama fulani. Askofu unaonekana kama chama fulani, mfano mimi ni mwanaccm nina dhambi zangu nataka kuja kuungama kwako, ntaungamaje kwako wakati wewe una itikadi tofauti na mimi?

Chama chetu kinaamini binadamu wote ni sawa, kinaamini katika utu, kinaamini katika kujitegemea, kinaamini katika heshima ya watu, kinaamini katika kusema kweli, kinaamini katika vita dhidi ya rushwa, kinaamini katika umoja kinaamini katika kujitoa, kinaamini katika kazi ni kipimo cha utu.

Sasa nikikutizama wewe unaamini katika ubwanyenye, unamini katika kuhodhi mali, unaamini katika umangimeza, unaamini katika mimi ni mwenyekiti peke yangu na hakuna mwingine. Sasa utaanza kunipoteza.
 
Nyie mnafikiri ndio wenye akili tu katika Watanzania mil 55? Yaani watu wakiwaambia uhuni wenu ambao uko waziwazi mnasema ni wa chama fulani? Kweli? Siyo Tanzania ya leo. Hata Maaskofu wakinyamaza, Watanzania wa kawaida watasema katika unyonge wao. Hamtofanikiwa kutawala kwa miaka 10 kwa mkono wa chuma. Jaribuni muone. Watanzania watadai shingo zenu kwa nguvu. Dunia imebadilika.
 
Fikra za hovyo sana,yani hawa wanajiaminisha kila anayepinga hii serikali ni chadema au amehongwa na mataifa ya magharibi.
Three(3) stages of truth-Arthur Schopenhauer
1.denial
2.violently opposition
3.accepted as being self evident
Hawa wako stage number 2 bado kidogo tu watakubali
Maaskofu hapo hapo mlipo shikilia.
Mkigeuka huku maaskofu,mara chadema,mara "the economist",mara ndege imeshikwa Canada,mara maandamano,Mara Mkapa anataka mjadala wa kitaifa kuhusu elimu.
Acceptance stage is around the corner
 
NNimeamini bongo kuna vilaza wengi sana maana watu wengi wameshindwa kugundua hizi kelele na haya maazimio yanatokana na nini?? Bongo lala mnaona kawaida tu Hii ni vita ya kiuchumi nyumbuu nyie angalieni huko mbele. Hivi mnafikiri watu wa nchi jirani na hao watu wa makinikia na madawa ya kulevya wanaitakia hii nchi mema?? Ila kwa vile wabongo wengi vilaza wanafuata mkumbo tu hawajui hata hawa wanaowachochea wanataka nini. Za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Mbona mnatuletea mambo ya zamani kujibu tuhuma za jama tena mwaka huu kuhusu hizi waraka mbili za Maaskofu wa Katoliki na KKKT?

Polepole kajibu zamani sasa ajibu tena, na mara nyingi nimesali naye KKKT
Watu wanapotea
wanapigwa risasi
hakuna kukosoana ni jela tu km Sugu huko Mbeya
watu kukamatwa kwa kutoa maoni km Mwl huko Bukoba
 
Maaskofu Hawa walishikwa kichwa na mbowe ziro watalipeleka taifa kubaya na matamko ambayo hata hawakubaliani

Wacha ubwege wako wewe mtoto wa shetani
 
Back
Top Bottom