nessonlegend
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,698
- 1,507
“HUMAN ZOO” - Historia iliyosahaulika
Hakuna mwalimu mzuri kama historia, kwa kadiri unavyozidi kuitafuta ndivyo unavyopata fursa ya kufahamu mambo mengi. Katika shule zetu kwa kiasi kikubwa tumefundishwa historia ya ukoloni barani Afrika, lakini hakuna mahali tulipofundishwa namna ukoloni huu ulivyoendana na biashara ya “MAONYESHO YA BINADAMU”
“Human zoo” ni biashara iliyoanza katika kipindi cha karne ya 16-20 mwanzoni (kwa mijibu wa vyanzo mbalimbali) ni biashara ambayo binadamu kutoka Afrika, walikuwa wakiwekwa katika majumba, vijiji, au katika maeneo mengine yaliyotengwa kwa lengo la kuonyeshwa kama bidhaa nyingine katika maonyesho ya (saba saba au nane nane). Biashara hii ilianza kukua kwa kasi hususani karne ya 17 yaani miaka ya 1600s ambapo wazungu wengii walikuwa wakituma wafanyabiashara Afrika kuja kununua watu kwa ajili ya maonyesho hayo. Pamoja na kwamba ilikuwa ni ukatiri mkubwa kwa wa afrika ila kwao ilikuwa ni kivutio cha maana sana kwani kwa kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo watazamaji walikuwa wakiongezeka toka sehemu mbalimbali kushuhudia asili ya mtu mweusi.
Katika biashara hii wa afrika walikuwa wakifanyiwa maonyesho ama wakiwa watupu (uchi) au nusu uchi (kwa kufunika sehemu za sili), katika maonyesho haya yaligawanyika katika makundi tofauti tofauti ambapo kuna waliokuwa wakionyeshwa kama familia nzima, au mtu mmoja mmoja ambapo alikuwa akionyeshwa uwezo wake, ukatili wake na mambo mengine kama hayo,watu wafupi (dwarf), pia walionyeshwa watoto wakiume na wakike ambapo walikuwa wakipewa ndizi kama vile tuendavyo kuangalia nyani au sokwe. Ni ukatili mkubwa japo kwao ni furaha iliyoje.
Moja kati ya stori ya kusisimua ni ya Ota Benga huyu alikuwa ni mwafrika aliyenunuliwa na mmishonari na mgunduzi Dr Samuel Philips Verner na kupelekwa USA mnamo mwaka 1904, inasemekana Verner alimleta Benga akiwa na watu wengine saba na kijana mdogo toka Kongo ambao walinunuliwa toka kwa mfanyabiashara wa watumwa ambapo familia ya Benga yani mke na watoto wake waliuliwa katika mauaji ya halaiki (massacre). Historia inasema kwamba, ujio wa Benga na wenzake ulikuwa kivutio kikubwa kwani katika kipindi hiki biashara ya utumwa ilikuwa imefifia sana na hivyo maonyesho yaliyodumu kwa muda wa miaka 400 yalikuwa yamepoteza mvuto kwa kukosa bidhaa (binadamu). Kundi la Benga na wenzake walikuwa wakisafirishwa kimaonyesho kwenda sehemu mbalimbali ikiwemo toka St louis, New orleans, Mardi glas na kisha kufika mpaka Afrika. Katika kuzunguka kote huku inasemekana Benga alionyesha juhudi ya kutaka kujua kusoma na kujifunza mambo ambapo alikuwa akimuomba Verner kumrejesha nyumbani Afrika.
Mnamo mwezi wa nane mwaka 1906 Verner na Benga walifanikiwa kufika New York, ambapo Verner alikuwa akitafuta sehemu ya kumuweka Benga ili aishi huko. Hatimaye akafanikiwa kumpeleka katika Bronxy zoo ambapo mwanzoni alikuwa akitembea tembea na kuwasaidia wafanyakazi wa zoo hiyo. Lakini mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka huo huo ikaamuliwa Benga apelekwe katika Orang Utan cage ambapo alikuwa akihamasishwa kucheza na jamii hiyo ya Orang utan na kufuma kofia pamoja na kuchezea mshale na upinde. Cage hii ilikuwa ikisimamiwa na Madison Glant huyu alikuwa ni New York Zoologist. (Masimulizi haya yapo katika kitabu cha Ota Benga, The Pygy in the zoo, kilichoandikwa na mjukuu wa Verner, Philips Bradford)
Pamoja na kuwepo kwa ukatili wa binadamu hususani asili ya watu weusi uliokuwa ukifanywa na wamishionari, lakini pia kulikuwa na kundi la watu waliokuwa wakipinga biashara ya maonyesho ya binadamu kama iliyokuwa kwa biashara ya utumwa. Dr Robert Stuart MacArthur of the Calvary Baptist Church in New York was outraged and was quoted in The New York Times on Sept. 10, 1906 as saying, ‘The person responsible for this exhibition degrades himself as much as he does the African. Instead of making a beast of this little fellow, he should be put in school for the development of such powers as God gave to him. It is too bad that there is not some society like the Society for the Prevention of Cruelty to Children. We send our missionaries to Africa to Christianise the people, and then we bring one here to brutalise him.’
“Mtu anayejihusisha na maonyesho haya, anajishusha yeye mwenyewe kama vile anavyowafanyia wa afrika, badala ya kumfanyia mambo hayo ilitakiwa tumpeleke shule akajifunze kwa kadili ya uwezo wao waliopewa na Mungu, ni jambo baya sana kwa jamii inayopinga unyanyasaji na ukatili kwa watoto, iliyotuma wamishonari Afrika kwenda kuhubili, kisha kuja na watu haohao na kuwafanyia ukatili” (tafsiri hii ya kimaana ni yangu).
Haya ni maneno yaliyotolewa na kasisi aliyekuwa ana asili ya Afrika-Amerika. ‘Our race, we think, is depressed enough without exhibiting one of us with the apes,’ wrote one such minister, James H. Gordon to the mayor of New York. ‘We think we are worthy of being considered human beings, with souls.’ Gordon was to become Ota Benga’s guardian after the zoo ultimately bowed to public pressure and had Benga removed.
Baada ya Benga kuwa chini ya usimamizi wa Gordon, alihamishiwa katika makazi yaliyojulikana kama Howard Colored Orphan Asaylum yaliyokuwa yamefadhiriwa na kanisa. Mnamo january 1910 Gordon akamfanyia Benga mpago wa kwenda Lynchburg, Virginia. Wakati huu Benga alikuwa akizungumza kiingereza kwa ufasaha huku akiwa anavalia mavazi ya kimarekani, baada ya kufika Virginia na hatimaye akaanza kufanya kazi katika kiwanda cha Tumbaku cha Lynchburgy. Pamoja na kwamba alikuwa na umbo dogo kuliko wafanyakazi wengine, alijidhihirisha kuwa ni wa kipekee hasa katika kupanda juu ya poles kufuata tumbaku bila ya kutumia ngazi, wenzake wakaanza kumwita Bingo. Alijihusisha na kusimulia historia ya maisha yake na alikuwa akipewa bia na watu kama shukrani ya simulizi yake. Katika kipindi hiki alikuwa na plani ya kurudi nyumbani Congo, lakini baada ya kutokea kwa vita ya kwanza ya dunia ndoto yake ikawa imefifia kwa kiasi kikubwa. Mnamo tarehe 20-3-1916 Benga akiwa na umri wa miaka 32 aliamua kukatisha uhai wake kwa kutumia bastola (pisto) aliyokuwa ameiba, kwa kujilipua upande wa moyo wake so sad kwa kweli. Cheti chake cha kifo kimeandikwa OTTO BINGO.
Maonyesho yaliyofanywa na Jesuits huko hispania barcelona 1929
Picha ya Roshina, mwanamke toka Guinea “malkia wa kwanza” wa maonyesho ya kireno huko Oporto mwaka 1934
Maonyesho ya kikoloni huko paris 1906
Mchoro wa saartije baartman huko makumbusho ya uingereza
Watot waliokuwa wakihifadhiwa kwa maonyesho hapo akipewa ndizi na watazamaji
Namna ambavyo walikuwa wakifanyiwa waafrika wenzetu.
Historia ni ndefu sana waweza kujiongeza kwa kutafuta maarifa zaidi kwa ku-google HUMAN ZOO