Mijitu mingine bwana!
Hivi wewe kwa akili yako unategemea hawa waliomteka Dr.Ulimboka ni watu waliotumwa na ndugu zake wanaogombea shamba kweli???Mimi siyo mwanasheria lakini hata Mahakamani kuna kitu wanaita,''circumstancial evidences'' au ushahidi wa kimazingira. Huo tu unatosha kumtia mtu hatiani. Sasa hebu tuangalia mazingira ya kutekwa kwa Dr. Ulimboka: Kwamba alipigiwa simu na mtu wa serikali(siyo ndugu yake,jamaa au rafiki) kwamba wakutane Leaders Club.Wakti wakiongea wakaja wale jamaa(agents) wakiwa na silaha(not majambazi) yumkini ni plain cloth policemen au Usalama wa Taifa na wakadai wanamtaka Dr. ULIMBOKA TU. Kilichofuatia hapo tunakielewa mpaka kuja kuokotwa kwa Dr. Ulimboka toka msitu wa Mabwepande.
Lakini pia wakti wa harakati za kumfikisha Dr. Ulimboka pale MOI baadaye walimbaini askari mmoja akiwa
CHOONI AKIWASILIANA NA WENZAKE SOMEWHERE KWA RADIO CALL AKIWAELEZA KUWA JAMAA(DR.ULIMBOKA) HAJAFA BADO ANAPUMUA!!!Hapa haihitaji hata akili ya kwenda kusomea sheria kila kitu kiko wazi.
Kama ni askari Polisi uko kwenye kutimiza wajibu wako KWANINI UKAONGELEE CHOONI??Ni dhahiri hawa walikuwa
Government AGENTS WALIOKUWA WAMEPEWA MAELEKEZO MAALUMU YA KWENDA KUMKAMATA NA KUMWUA HUYU DOC ILI KUMNYAMAZISHA KWA KIFO!!!Huo ni ukweli ambao kila mtu mwenye akili timamu atakubaliana nao.
Mimi kwa mawazo yangu ni kwamba tunataka haya 3 yafuatayo yafanyiwe kazi kwa haraka sana:
- Huyu kigogo wa Serikali aliyemwita Dr. Ulimboka wakutane Leaders Club ni nani na awe wa kwanza kukamatwa ili aisadie polisi.Huyu atakuwa anajua mchongo wote.
- Yule askari alyekuwa anawasiliana na wenzake kuwajulisha kuwa Dr. Ulimboka hajafa naye akamatwa kama yule kigogo.
- Kuundwe tume huru itakayohusisha pande zote mbili MADAKTARI,SERIKALI(POLISI)na KAMATI YA BUNGE YA HAKI ZA JAMII ili kufanya uchunguzi wa kina kabisa kuhusu sakata hili. Kama POLISI wataachwa peke yao washughulikie hili tatizo basi tusitarajie matokeo mazuri! Maana kama kweli kuna mkono wa serikali LAZIMA WATACHAKACHUA TU!We really know them.
Wasalaam.