kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,585
- 14,045
Kumhukumu mtu kwenda jela na baadaye mtu huyo kushinda rufaa kunasababisha chuki zisizokwisha kwa waathilika wa hukumu hizo pamoja na wafuasi wao. Unasababisha mateso yasiyo ya lazima kwa mtu, familia, ndugu na marafiki. Huku ni kupanda mbegu mbaya ya chuki na visasi mioyoni mwa watanzania. Matukio haya ya kushinda rufaa yanayozidi kuongezeka nchini yanamaanisha nini? ni Elimu ya sheria imeshuka hivyo kuzalisha mahakimu vilaza au kuna rushwa kwenye hukumu au siasa inaingilia hukumu hizi?. Utafiti wa kina unahitajika hapa ili kulijua tatizo.