Hukumu za Mahakama Kuu

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,357
6,422
Kwa nia njema tu kabisa nauliza:(na si kwa kubeza au vinginevyo): Kwa nini hukumu nyingi (si zote nisisitize) za Mahakama kuu zikienda Mahakama ya rufaa huwa zinatenguliwa? Nimefanya utafiti usio rasmi na kujiridhisha kuwa iko hivyo. Kesi hasa za mauaji, rape , economic crimes (list not exhaustive).
Nadhani kuna tatizo la msingi ambalo idara ya mahakama iliangalie kwa nia njema tu ya kuboresha utoaji haki
 
Mahakama kuu kuna VODA FASTA wengi; lakini kule kwenye MAHAKAMA YA RUFAA hawa wa voda fasta kupenyeza sio rahisi!! Hukumu pia hutolewa na majaji na sio jaji!!!!
Napendekeza, Mahakama kuu kuwe na utaratibu wa kuwa na majaji wawili katika kusikiliza kesi na kutoa hukumu. I am alive aware kuwa Mahakama ya Rufaa huwa ni majaji 3, (lazima kuwe na odd number kwa ajili ya kupata majority) hii itatoa nafasi ya wawili kusaidiana kufikia uamuzi sahihi according to the dictates of law!
 
Majaji wakiwa zaidi ya mmoja Mahakama kuu ni nzuri lakini kuna tatizo la kuchelewa kwa kesi linaweza kujitokeza.

Jaji Mmoja akiugua kesi inaahirishwa, hadi baada ya mwezi mmoja. Akija mwenzake kaenda likizo, kesi inaahirishwa.

Mpaka usikilizwe umeshakoma.
 
Back
Top Bottom