Hukumu ya Zombe: Aachiwa!

Tatizo lipo kwa wapelelezi hawawezi kabisa kutafuta ushahidi muafaka. Wapelelezi wameshindwa kutafuta habari za wale jamaa waliokimbia (kama siyo kuchinyiwa baharini), wameshindwa kumlinda shahidi muhimu afande Lema mpaka akafariki kiutatanishi akiwa mikononi mwa mahakama (remand). Sasa Zombe atakamatwa kwa ushahidi upi? he is damn clean. Ingawa ndiye muuaji mkuu.
 
Of course Zombe atachomoa... dalili zilionekana mapema toka wazee walipomuona hana hatia.

Ila ndo sheria jamani
 
Duh na Lema ndio alikuwa shahidi muhimu, basi watatoka kina Zombe.
Ndo hivyo tena, Jaji ameutupilia mbali. Anasema hayo maelezo ya Lema hayawezi kuisaidia Mahakama kuwatia hatiani watuhumiwa kwakuwa hayupo kishakufa!
 
Mambo yangeweza kumuwia magumu zombe kama watuhumiwa wengine wangekuwa na ushahidi wa kuthibitisha kama waliyotenda yalikuwa ni kwa maelekezo yake. Anaweza kuwa na hatia kwenye mambo mengine madogo madogo, lakini sio suala la mauaji, kwani hakuna ushahidi wa kumhusisha kufika kwenye eneo la tukio.
 
Mshitakiwa wa 12 (Rajabu0 nae alikuwa na ushahidi muhimu. Nadhani maelezo yake bado yana umuhimu wa aina yake
 
Hata kama ZOMBIE ataepuka hii hukumu ya mwanadamu ya Mungu ambaye ni ndiye judge wa kweli mwenye utimilifu usio na mipaka ZOMBIE/ZOMBE ataipata huko.
 
Kwa jinsi mambo ya navyo kwenda kuna kila dalili Zombe akawa huru mda si mrefu.
 
Chenge mjumbe kamati ya maadili CCM na mkapa naye ni mjumbe wa kamati ya maadili CCM. pazia likapasuka pwaaaaaa nao wakacheka yote sawa hakuna haki mambo yote udhalimu chini ya jua.

pop corn zimeisha sinema bado haijaisha.
 
Wakuu muda kidogo pls, tuna mwandishi yupo mahakamani anatu-update kila kinachoendelea lakini mpaka sasa Jaji anaendelea kuchambua ushahidi. Hatuwezi kuandika kila anachoongea lakini matokeo ya alichoongea (maamuzi) ndiyo rahisi kuandika.

LAZIMA tujue hatma ya kesi hii leoleo, tena ndani ya masaa 2 yajayo!
 
Nilisha waambia kuweni makini mahakama ndo mwamuzi wa mwisho kwenye hili game.
 
kweli zombe anasubiriwa hii thread ina jam balaa,kila raia anawait awe wa kwanza kuvunja habari, duh!!
 
Back
Top Bottom