Hukumu ya shambulio la Westgate 2013 yatarajiwa kutolewa leo kwa watuhumiwa waliohusika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Hatma ya washukiwa wa shambulizi dhidi ya jengo la Westgate kujulikana Jumanne hii

Hukumu ya washukiwa wa mlipuko wa kigaidi katika jengo kubwa la maduka la Westgate jijini Nairobi mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 67 inatarajiwa kutolewa leo Jumanne baada ya kuahirishwa jana.

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amesema kuna mambo yalikuwa hajakamilika, na hivyo kulazimika kuahirisha uamuzi huo kwa mara nyingine.

Watu 67 waliuawa katika shambulio hilo ambalo wanamgambo wa kundi la al-Shabab walidai kulitekeleza.

Kundi la Al-Shabab linaendelea kuwa tishio kwa usalama wa kanda hii kutokana na jinsi limekuwa likibadilisha mbinu ya mashambulizi katika taifa jirani la Somalia ambalo ndio chimbuko lao.

Kundi hilo liliimarisha mashambulizi yake kufuatia hatua ya Muungano wa Afrika, kupeleka kikosi chake cha kulinda amani AMISOM, nchini Somalia kwa ushirikiano na Marekani.

Kundi hilo lilifurushwa kutoka mji mkuu wa Mogadishu, mwezi Agosti 2011 kufuatia uvamizi uliotekelezwa na wanajeshi 22,000 wa Muungano wa Afrika na kuondoka katika bandari muhimu ya Kismayu mwezi Septemba 2012.

Wakati lilipoondolewa katika bandari ya Kismayu kundi hilo lilipoteza fedha nyingi kwa kuwa lilikuwa likijipatia fedha hizo kupitia uuzaji wa makaa.

RFI Kiswahili
 
Back
Top Bottom